Habari za Punde

Masheha watakiwa kusimamia vyeti vya Mazao

Mkurugenzi Mwezeshaji Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Bakari Haji akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid kufungua Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la Karafuu ,katika  Ukumbi wa Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 febuari 2023. 
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid  akizungumza na Wadau na Wakulima wa Zao la  karafuu Wakati alipokua  akifungua mkutano wa Wadau hao   ulioandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa  Zanzibar ZSTC   huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati   Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 fubuari 2023.
Katibu wa Shirika la Biashara laTaifa  Zanzibar ZSTC  Ali Hilal Vuai (alieshika kinasa sauti) alipokua akitoa tathmini ya utekelezaji wa kazi za Shirika wakati wa mkutano na Wadau na Wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa kusini Unguja, tarehe 26 so fubuari 2023 
Katibu wa Jumuiya  ya Wakulima wa zao la  karafuu (ZACPO)  Salim sleyum abeid alipokua akitoa salamu za Jumuiya katika mkutano wa wakutathmini zao Hilo Kwa mwaka 2022-2023 uliowashirikisha Wadau na Wakulima huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.
Wadau na wakulima  wa Zao la  Karafuu  walipokuwa katika Mkutano wa kutaathmini zao Hilo Kwa mwaka 2022-2023 ulioandaliwa na Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar ZSTC na kufanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 fubuari 2023.
Afisa kutoka Wizara  ya Kilimo Mussa Rajabu alipokua akihamasisha upandaji wa miche ya mikarafuu katika  Mkutano wa Wadau na Wakulima  wa Zao hilo uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023
Afisa masoko Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Aziza Baraka Omar   alipokua akitoa  elimu ya malipo na kutunza fedha  kupitia Benki hiyo wakati wa Mkutano wa wakulima na Wadau wa Zao la Karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.
Meneja wa Tigo pesa  Zanzibar Salum Nassor alipokua akitoa elimu kuhusiana na malipo kupitia Ezypesa -Tigopesa wakati wa Mkutano wa Wadau na wakulima wa Zao la Karafuu uliofanyika Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati  Mkoa wa Kusini  Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.
Sheha wa Shehia ya Bambi Amour Mkombe  alipokua akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26,fubuari 2023.
Mkulima wa zao la karafuu Shehia ya Dunga bweni Abdalla Khamis Sadala akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26,fubuari 2023.

Mkulima wa zao la karafuu Bungi Khamis Malik khamis  akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023

Mkulima wa zao la karafuu Shehia ya Koani Rukia Abdalla Mwinyi akichangia mada katika Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la karafuu uliofanyika skuli ya Dunga Mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 26 fubuari 2023.

( PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

 

Na Rahma Khamis Maelezo                      26/2/2023

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Masheha wa Mkoa huo kusimamia vizuri utoaji wa vyeti vya mazao hasa zao lakarafuu ili wakulima waweze kuuza bizaa zao kwa urahisi zaidi.

Wito huo ameutoa huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati katika mkutano wa wakulima na wadau wa karafuu wa kutathmini changamoto zinazowakabili wakati wanapokwenda kuuza karafuu zao katika Shirika la Biashara (ZSTC)

Amesema kuna baadhi ya masheha hawawajibiki ipasavyo katika kutoa vibali kwa wananchi jambo ambalo linawakosesha fursa wakulima kusafirisha bizaa zao kwa ajili ya mauzo ili kujikimu na maisha.

Aidha amefahamisha kuwa Serekali inaendelea kutegemea zao la karafuu katika kuongeza pato la nchi hivyo ipo haja ya kuliendeleza,kulitunza na kulithamini zao hilo kwa maslahi ya Taifa na wnanchi kwa ujumla.

Mkuu huyo ameinasihi Wizara ya Kilimo kuendelea kuvitunza vitalu vya miche ili wakulima wanufaike kwani miche hiyo ni muhimu katika kuendeleza kilimo cha zao hilo.

Akizungumzia suala la uaminifu kwa wakulima Mkuu huyo amesema kuwa kuna baadhi ya wakulma wanajitoa uamnifu kutokana na kuchanganya karafuu na makonyo wakati wa kuuza ili kujiongezea kipato jambo ambalo linapelekea kuondoa haiba ya zao hilo.

Hata hivyo amewashauri wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa makini katika kulilinda,kulitunza zao hilo kwani kuna baadhi ya watu wanaweza kuingiza karafuu kutoka nje ya nchi kinyemela na kushusha hadhi ya karafuu ya Zanzibar.

Nae Katibu wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Ali Hilali Vuai amesema kuwa miongoni mwa tathmini ya kazi zao ni kununua karafuu kutoka kwa wakulima ambapo kwa mwaka 2022/23 wamenunua tani 3785.000 zenye thamani ya Sh, 7151661000 za TZ.

 Aidha amefahamisha kuwa wamefanikiwa kununua karafuu ambazo hazijachanganywa na makonyo kwa mwaka huu kutokana na kununua mashine za kuchujia na kusema kuwa changamoto inayowakabili ni baadhi ya wakulima kupeleka karafuu ambazo hazijakauka vizuri jambo ambalo sio sahihi.

 Kwa upande wao wakulima wa zao hilo wamesema ukosefu wa visima katika maeneo ya mashamba ya mikarafuu imepelekea baadhi ya miti hiyo kufa kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.

Aidha wamiomba Wizara ya Kilimo kufanya utafiti wa ardhi ambayo itaweza kuota mikarafuu kwa ili zao hilo lipandwe kwa wingi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.