Habari za Punde

Airtel Tanzania yafuturisha waislamu na wakristo

Mkurugenzi Mtendaji wa Aitel Tanzania, Dinesh Balsingh ( kulia) na Mkurugenzi wake wa Biashara wa Aitel, Amit Chandiraman wakigawa  futari kwa wafanyakazi wa  kampuni hiyo katika hafla waliyowaandalia kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kwaresma kwa wakristo  jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Kitengo cha Mauzo wa Airtel Tanzania, Dominician Mkama  akigawa tende katika hafla ya futari waliyoiandaa Kwa  wafanyakazi wao kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma Kwa wakristo  jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Kitengo cha Rasilimali Watu wa Aitel Tanzania, Stella Kibacha akigawa mlo wa  futari  katika hafla waliyoiandaa Kwa  wafanyakazi  kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kwa wakristo  jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Biashara wa Aitel Tanzania, Amit Chandiraman akigawa  mlo wa futari  katika hafla  iliyoandaliwa kwa wafanyakazi wao   kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kwa wakristo   jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na kampuni yao katika kipindi hiki cha Mfungo Ramadhani kwa waislamu na Kwaresma kwa wakristo jijini Dar es Salaam jana.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imeandaa hafla ya futari Kwa wafanyakazi wake waislamu na wakristo ikiwa ni ishara ya shukurani na pia kudumisha umoja na mshikamano baina ya wafanyakazi hao.

Akizungumza wakati wa hafla huyo, mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bwana, Dinesh Balsingh  alisema hafla hiyo imekuwa ya baraka mno ukizingatia kuwa kipindi hiki waislamu kote nchini wanaendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hali kadhakika waumini wa dini ya kikristo wao wakimaliza mfungo wao wa Kwaresma.

"Sisi kama Airtel Tanzania tunaamini mshikamano mahali pa kazi ndio siri kubwa ya mafanikio yetu, hivyo hafla kama hizi ni muhimu sana katika kuendelea kuwaweka wafanyakazi pamoja na kudumisha moyo wa upendo, umoja na mshikamano miongoni mwao.

"Kwa namna ya kipekee tungependa kuwashukuru wafanyakazi wote wa Airtel kutoka katika Kila idara, wafanyakazi wa kada zote kwa jitihada zao bila kuchoka katika kuwahudumia wateja wetu, wao ndio siri ya ubora wa mtandao na huduma zetu bora, ni matumaini yetu kuwa jitihada hizo na uchapakazi wao utaendelea kuiweka Artel Tanzania kileleni linapokuja suala la huduma bora za simu za mkononi nchini", alisema Bw, Balsingh

Aidha Bwana Balsingh alisema Airtel Tanzania inawatakia wafanyakazi wake wote pamoja na wateja wake heri ya msimu wa sikukuu za Pasaka zinazoanza kuadhimishwa na wakristo wote duniani kuanzia Ijumaa hii ya April 7 hadi Jumatatu April 10 huku ikiendelea kuwatakia mfungo mwema wa Ramadhani waumini wa dini ya kiislamu.

"Pamoja na hayo tunawatakia  watanzania wote  Sikukuu njema ya Pasaka  na mfungo mwema wa Ramadhani huku mkiendelea kufurahia mtanda bora kila mahali, bidhaa na  huduma zetu bora za mtandao wetu wenye nguvu pamoja na ofa lukuki, vifurushi kabambe bila kusahau zawadi bomba zinazotolewa kupitia  kampeni zetu mbalimbali zinazoendelea. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.