Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameongoza Wananchi wa Zanzibar Katika Kisomo cha Dua Kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kabla ya kuaza kwa Kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume, dua hiyo iliyofanyika leo 7-4-2023 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Hemed Suleiman Abdulla
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongoza kisoma cha hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume, iliyofanyika leo,7-4-2023 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi


NAIBU Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi (wa kwanza ) akijumuika na Wananchi katika kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mareheme Sheikh. Abeid Amani Karume, iliyofanyika leo 7-4-2023 katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
SHEIKH.Jaffar Abdalla Ramadhan akihitimisha kisoma cha Hitma na dua, ya kumuombea  Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika katika kuitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume iliyofanyika leo 7-4-2023,katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na ((kulia kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dkt. Amani Karume na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
IMAMU Mkuu wa Msikiti wa kwa Mtoro Dar es Salaam Sheikh. Abass Ramadhan akitowa mawaidha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, baada ya kumalizika kwa dua na kisomo cha hitma cha kumuombea marehemu kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja 

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume,iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja leo 7-4-2023 na (kulia kwa Mufti) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj.Dkt. Amani Karume na (kushoto kwa Mufti Mkuu ) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.

BAADHI ya Wananchi waliohudhuria kisoma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume, wakiitia dua ikisoma na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) kisomo hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa dua na kisomo cha hitma cha kumuombea marehemu kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.



 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.