Na.Rashid Omar. -OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman, amesema kwamba kufuata maadili
na sheria za kazi kwa watumishi wote wa umma ni jambo muhimu katika
maendeleo ya nchi kwa vile maadili na Usalama kazini ndio roho
na moyo wa Utumishi wa umma katika nchi yoyote duniani.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko ukumbi wa Sheikh Idrisa Abduli- Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar alipofungua mafunzo
ya watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais
Zanzibar kuhusu maadili ya kazi na usalama kazini.
Mhe. Makamu amefahamisha kwamba utumishi wa Umma Zanzibar
umeanza miaka kadhaa iliyopita kwa
kupitia katika hatua mbali mbali na kwamba iwapo nchi inataka kujenga utumishi
bora ni vyema pia kuangalia na historia.
Amesema kwamba Zanzibar wana kila sababu ya kuutunza na
kuufanya utumishi wa umma utukuke kutokana na historia yake iliyoanzia mwaka
1890 kwa kuanza mfumo rasmi wa serikali ambapo ndipo serikali ilipoanzishwa
chini ya himaya ya utawala wa Kingereza na marekebisho yake sheria na kanuni
hizo yakafanywa tangu 1906 na baadaye 1924.
Amefahamisha kwamba mfumo rasmi ulioweka mawaziri ulikuja
mwaka 1960 na kukatolewa muongozo na sheria za jumla za utumishi ulioweka wajibu,
kwa viongozi mbali mbali wakiwemo watumishi , viongozi mawaziri na wakurugenzi
sambamba na kuwepo Kamisheni ya Utumishi wa umma kusimamia utumishi wa
kiserikali.
Mhe. Makamu amewataka watumishi wa umma Zanzibar kufanya kazi
kwa kuzingatia wujibu , taratibu na kanuni za kiutumishi za leo ambazo
unakwenda na mfumo wa Kikatiba katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa haraka.
Amesama licha ya utumishi wa umma Zanzibar kupita katika
vipindi vingina hatua mbali mbali ni vyema sasa kuelekeza utumishi huo kulingana na katiba sheria na katuni za
nchi kwa kuwa ndio vinavyoongoza
utumishi huo sambamba na kuzingatia utamaduni wa sasa wa kuendesha nchi.
Amesema kwamba Zanzibar kwenye utumishi wa umma umepita
katika vipindi tofauti na kwamba sasa jambo muhim u ni kuwepo mfumo
wa kikatiba wa utumishi na kwamba dunia
ya sasa inazingatia ushindani katika kuendesha nchi na kwamba ukiwa na serikali
isiyokuwa na ufanisi huwezi kupata maendeleo na kuwataka watumishi na viongozi
kuzingatia hilo ili taifa liweze kusonga mbele .
Amewataka watumishi na viongozi kuhakikisha kwamba wanafuata
maadili kutokana na umuhimu wake hasa katika utoaji wa huduma kwa uaminifu
mkubwa wa kimaadili.
Amesema kwamba watu wanotumikiwa wanaawaminisana viongozi kutokana na imani ya kuwepo maadili
mema waliyonayo watumishi na kwamba yasipozingatiwa uaminifu na imani kwa
wanaotumikiwa itapotea.
Amesama kwamba upo uhusuinano mkubwa baina ya maadili na kumtengeneza mazingira ya kuamini katika
kazi tunazofanya na kujengea imani
wanaoutumikiwa ambao ni wananchi na kwamba ni jambo la muhimu sasa
kushikamana na maadili.
Amewataka viongozi
wote kuzingatia sana uwezo , tabia na mwendendo mwema binafsi wa mtumishi tangu wakati ajira yake kwa kuwa wanaoajiriwa bila kuwa na maadili
tokea awali sio rahisi kuwa na kuzingatia maadili katika mahala pa kazi.
Amewataka watumishi na viongozi kuachana na imani zao za siasa
wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mbali mbali ya kiutumishi kwa kuwa bila kufanya hivyo ufanisi wa kazi hautopatikana.
Amesema kwamba kuchanganya imani za kisiasa katika utumishi
wa umma ni dhambi kubwa ambayo inaweza kuharifu mfumo na maendeleo ya kazi huku
kukuwepo idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji kuhudumiwa hawana ufuasi wa vyama
.
Amewataka watumishi
kuacha kuchanganya siasa za vyama na
kwamba hapa Zanzibar hali hiyo imechangia sana kuharibu utumishi wa umma na
kwamba ni wajibu wa viongozi na watumishi warudi kwenye mstari kwa kutotumia imani za siasa katika
kutekeleza majukumu yao.
Aidha amewataka viongozi kufahamu kwamba ni walizi wa haki za
watumishi wote na kwamba hata iwapo mtumishi haijui haki yake kiongozi
anawajibu wa kuhakikisha kwamba haki hiyo imepatikana kwa kudaiwa ama hata kwa
kutodaiwa na mtumishi mwenyewe.
Naye waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais Mhe. Harous
Said Suleiman, amesema kwamba mafunzo hayo ni katika fursa muhimu kwa watendaji
na wafanyakazi nchi katika utoaji wa
huduma na kujenga ufanisi katika kuutumikia umma.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Omar Dad Shajak amesema kwamba
mafunzo hayo yanalenga kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kuhakikisha
kwamba watumishi wote wa umma wanapatiwa taaluma juu ya sheria, maadilini na usalama kazini.
No comments:
Post a Comment