Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amejumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba Katika Futari

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari aliyowaandalia katika ukumbi wa Tibirinzi Chakechake Pemba, akiwa na Viongozi wa Serikali na Chama. 

Na.Ali Muhamed Shaban.OMPR

Kuwepo kwa umoja, mshikamano, upendo kwa viongozi na wananchi kutasaidia kupata maendeleo endelevu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na baadae.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Matar Zahor Masoud ameyasema hayo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba na Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyofanyika kwenye ukumbi wa ZSSF Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

 

Amesema umoja, mshikamano na upendo kwa Taifa lolote  duniani baina ya wananchi na viongozi ndio sababu ya Taifa kufikia malengo waliojiwekea hivyo, amewataka wananchi kuiga mwenendo wa viongozi wakuu kwa  kudumisha Umoja , upendo na mshikamano baina yao hasa kwa kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni kuendeleza umoja na mshikamano kwa wananchi ili kuweza kuwaletea maendeleo endelevu kwa maslahi ya  Taifa.

 

Alhajj Hemed amewataka wananchi kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee ,mayatima,wajane, watu wenye ulemavu pamoja na watu wasiojiweza ili kuweza kudiriki kutimiza ibada ya funga pamoja na kupata fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameendelea kuwataka wafanyabiasha kuwaonea huruma wananchi kuweza kupata huduma za chakula zinazotumika katika Mwezi Mtukufu na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kusimamia utaratibu wa upatikanaji wa bidhaa ili kuhakikisha wananchi wanatekeleza Ibada ya funga kikamilifu kwa kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi kupitia bei za bidha mbali mbali nchini.

 

Akitoa Shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba na Mkoa wa Kaskazini Pemba Sheikh OMAR HAMAD ALI amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuamua kujumuika na wananchi katika Iftari hiyo na kueleza kuwa jambo hilo linadhihirisha namna kiongozi huyo anavyowajali wananchi wake pia  linaongeza upendo baina yao na Imani kwa wananchi juu ya viongozi wao.

 

 

Ameeleza kuwa suala la kufuturisha waumini linaonesha namna kiongozi huyo alivyokuwa na uchamungu pamoja na kufuata kivitendo maelekezo ya Uislamu kupitia mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W)

 

Aidha sheikh OMAR amewataka wananchi kuendelea kuwaombea Dua Viongozi wa Serikali ya Awamu ya nane chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili kuweza kuwaongoza kwa upendo na kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa Zanzibar.


Ali Muhamed Shaban

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

08/04/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.