Na Rahma Khamis,Melezo 24.04.2023
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Islam Seif Salim ameliomba Shirika la Afya Duniani WHO kuendelea kuisadia Zanzibar katika kukabiliana na maafa pindi yanapojitikeza.
Ameyasema hayo katika Hoteli ya Visitor Inn Jambiani wakati alipokua akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Taasisi mbalimbali juu ya kukabiliana na maafa.
Amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Shirika hilo katika sekta mbalimbali hivyo ameliomba Shirika hilo kuendelea kuongeza nguvu ya kusaidia hasa katika kukabiliana na majanga yanayojitokeza ambayo huathiri jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha amefahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha nchi za kiafrika zinaweza kutumia rasilimali walizonazo katika kukabiliana na maafa pindi yanapojitokeza.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watendaji kuweza kukabiliana na maafa yanayoendelea kuathiri afya za watu ,miundombinu na mazingira siku hadi siku
"wakati yanapotokea maafa mambo mbaalimbali hujitokeza kama maradhi ya mripuko,watu kukosa makaazi na hata miundo mbinu kuharibika,hivyo mafunzo haya yatawawezesha waatendaji kuweza kukabiliana nayo wakati wowote yanapotokea" Katibu alisema.
Hata hivyo Katibu huyo aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kua na umoja na kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili jamii iwe salama.
Nae Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Andermichael Gihrmy amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na kushiriki ipasavyo katika mafunzo hayo ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Afya Mwatoum Ramadhan Mussa amewata washiriki kuwa wasikivu na watulivu wanaopatiwa mafunzo hayo ili kuitumia vyema fursa hiyo itakayosaidia kuweza kukabiliana na maafa yanapotokezea Nchini .
Mafunzo hayo ya siku 24 yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO ambapo yameshirikisha watendaji kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Mazingira, Maji, Ustawi waJamii na Maafa.
No comments:
Post a Comment