Habari za Punde

K0NGAMANO LA HABARI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa uchechemuzi  LHRC Maduhu William wakati alipokua  akitembelea maonyesho ya vitabu yaliokuwa nje ya Ukumbi wa Golden Tulip  wakati alipofika kuzindua kongamano la wadau wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya  Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani  huko Uwanja wa Ndege Zanzibar
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Kampuni ya Habari na Teknolojia Daniel Mwinjira wakati alipokua akitembelea maonyesho ya vitabu  yaliokuwa nje ya Ukumbi wa Golden Tulip  wakati alipofika kuzindua kongamano la wadau wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani  huko Uwanja wa Ndege Zanzibar
Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambae pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar  Hassan Khatib Hassan akizungumza machache wakati alipokua akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua kongamano la wadau wa Habari lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 
Waandishi wa Habari wabobezi walipokua  katika majadiliano kuhusiana na kuimarisha mchango wa Vyombo vya Habari katika kufikia maendeleo endelevu wakati wa kongamano la wadau hao lililofanyika Golden tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Dunian
Wadau wa Habari walipokua wakifuatilia kongamano la  Habari lililofanyika Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari duniani 
Wadau wa Habari walipokua wakifuatilia kongamano la  Habari lililofanyika Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari duniani 

Wadau wa Habari walipokua wakifuatilia kongamano la  Habari lililofanyika Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.

Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Mauli Mwita akizungumza na wadau wa Habari wakati alipokua akizindua kongamano la wanahabari kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani  huko Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar

Na Rahma Khamis  Idara ya Maelezo Zanzibar    1/5/2023

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Zanzibar Mhe Tabia Maulid Mwita amewataka wanahabari kufuatia habari kwa uhakika ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege wakati alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kuadhimisha miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Amesema habari ni kitu muhimu hivvyo wanahabari wana jukumu la kutoa taarifa sahihi kwa jamii na kujitahidi kufanya kazi zao  kwa weledi zaidi ili kutekeleza fani hiyo kwa ufanisi..
Waziri Tabia ameeleza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kulinda na kuangalia hali ya uhuru wa vyombo vya habari duniani pia Serikali inapata nafasi ya kukutana na na washiriki wake wa maendeleo na asasi za kiraia katika kukuza fani hiyo.

"Serikali ya Mapinduzi kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaahidi kuendelea kushirikiana na UNESCO ambayo ndio mfadhili kiongozi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani", amefahamisha Waziri huyo.

Waziri Tabia amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari inatoa fursa kwa watu duniani  kote hasa wanahabari kuonyesha mshikamano wao kwa kutoa wito wa kuondoa vizuizi vya kupata habari.

Ameeleza kuwa pia wanahabari  wanaweza kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi na Taasisi kwa kuwakumbusha watu kuhusu umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika kukuza maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

"Dunia hivi sasa inakabiliwa na uchafuzi wa mazingira ambayo chanzo chake ni wanadamu hivyo ni dhamira ya wazi kuwa maadhimisho hayo yameshirikiana kuhusu kukabiliana na tatizo hilo", amefahamisha.

Waziri huyo ameongeza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inatekeleza miradi mingi ikiwemo habari ni vyema wanahabari waweze kutoa taarifa hizo kwa usahihi na kuwafikia  wananchi kwa wakati.

Waziri amewasisitiza wanahabari kufuatilia changamoto za wananchi pamoja na kutoa taarifa za maendeleo ya nchi ili waweze kufahamu   hatua na yanayoendelea nchini.

Amesema kuwa maadhimisho ya siku hiyo yatatumika kama jukwaa muhimu katika kuibua changamoto za kisera pamoja na kuangalia uboreshaji wa mazingira ya uendeshaji wa vyombo vya habari  nchini.

Waziri Tabia amewatoa wasiwasi wanahabari hao  kuhusu kubadilishwa kwa sheria ya habari  kwani  Serikali inaendelea na mchakato huo na karibuni sheria hiyo itapelekwa  katika vyombo vya kutunga sheria kwa hatua.

Nae Mkurugenzi  wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatib Khasan  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari  Mhe Fatma Hamad Rajab akimkaribisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe,Tabia Maulid Mwita amewashukuru wale wote walioshiriki kufanikisha shughuli hiyo.

Nao washiriki wa kongamano hilo wamesisitiza wanahabari wenzao kujifunza kitaaluma ili kukuza fani hiyo na kufanya kazi kwa weledi na ufanisi

Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari hufanyika kila ifikapo Mei 3, kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu KUUNDA MUSTAKABALI WA UHURU WA KUJIELEZA KAMA KICHECHEO CHA HAKI ZA BINAADAMU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.