Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Maunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Khamis Abdalla : Asema Haridhishwi na Ufaulu wa Wanafunzi Nchini

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said,akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zazibar (V.T.A) katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo nje kidogo ya Jiji la Zanzibar huko Beit el ras, Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.

Na.Mwandishi Wetu -Zanzibar.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Zanzibar Khamis Abdullah Said, amesema uwekezaji wa Serikali katika sekta ya Elimu nchini hauendani na matokeo ya viwango vya ufaulu wa Wanafunzi wa ngazi mbalimbali za kielimu nchini.

Kauli hiyo ameitoa katika mwendelezo wa vikao vyake vya kukutana na Watendaji wa idara,bodi na vitengo vya Wizara hiyo huko Mazizini, Zanzibar.

Alisema Serikali ya awamu ya nane chini ya usimamizi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,ameweka mazingira rafiki ya kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayolenga kuongeza viwango ubora vya ufaulu kwa Wanafunzi vinavyoendana na hadhi ya Zanzibar kitaaluma.

Khamis, alieleza kuwa juhudi hizo zinatakiwa kuthaminiwa na kila mtendaji ndani ya taasisi hizo khasa Wakaguzi wa Elimu kuanzia ngazi ya Maandalizi,Msingi hadi Sekondari  ambao ndio wenye dhamana kubwa ya kuhakikisha nchi inakuwa na viwango bora vya ufaulu wa Wanafunzi katika mitihani ya ndani na Kitaifa kwa ujumla.

Aliwambia Wakaguzi hao kuwa wao ndio chimbuko la kupatikana kwa wanafunzi na skuli bora kwani kazi yao kubwa ni kukagua kwa kina hali halisi  ya maendeleo ya kitaaluma na kuandika ripoti zenye ushauri na mapendekezo ya  

Alifafanua kuwa tatizo la ufaulu mdogo linaanzia katika ngazi za elimu ya maandalizi na msingi ambapo wanafunzi wengi wanakosa kuandaliwa vizuri na matokeo yake wanaenda ngazi ya Sekondari bila kufikia viwango bora vya kuwawezesha kukabiliana na elimu ya Sekondari.

“Wakaguzi wa elimu kuanzia leo naomba mkatekeleze wajibu wenu kwa kukagua kwa kina huko Maskulini hasa ngazi za maandalizi na msingi hakikisheni mnagagua,kuchambua na kufanya utafti wa mbinu zinazotumiwa na Walimu kufundisha Wanafunzi, nina uhakika kuna mengi mtayaibua ya kujenga sekta ya elimu.

Binafsi siridhishwi na matokeo ya ufaulu kwa ngazi ya Msingi hadi Sekondari kwani hayaendani na hadhi ya Zanzibar kitaaluma, ni lazima tufanye kazi ya ziada kwa kuhakikisha mnasimamia vizuri dhamana mlizopewa”,alifafanua Katibu Mkuu  huyo Khamis.

Pamoja na hayo aliwaelekeza Wakaguzi hao kutumia taaluma zao kwa kuhakikisha wanagagua kwa uelezi na utafti kwa lengo la kuibua hoja za msingi zitakazoonyesha tatizo la kushuka kwa ufaulu ili mamlaka ya juu itafute ufumbuzi wa kudumu.  

Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo, alisema malengo ya Elimu yameandikwa katika Sera ya Elimu ya mwaka 2006 ambapo moja ya dhamira yake ni kumuandaa kijana kuwa raia mwema,mzalendo na mtiifu kwa nchi pamoja na kumuandaa na stadi za maisha zitakazomsaidia mwenyewe na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Katibu Mkuu huyo Ndugu Khamis Abdullah, alizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar (V.T.A) huko Afisi kwao Beit el ras,aliwasihi wajiandae kisaikolojia kutokana na taasisi yao itaongezewa majukumu ya kuwa mamlaka ya ubunifu na ujuzi kwa ajili ya kuinua viwango vya kitaaluma nchini.

Aliongeza kwamba kupitia taasisi hiyo itasimamia mitaala ya masomo mbalimbali yanayofundishwa maskulini kumjenga mwanafunzi kusomea fani inayoendana na kipaji chake.

Khamis, aliongeza kuwa kupitia mabadiliko hayo ya kielimu yatatoa fursa pana kwa Wanafunzi mbalimbali kuwa wabobezi katika fani mbalimbali zikiwemo zinatokana na dhana ya Uchumi wa Bluu wenye fursa nyingi za kumuwezesha mhitimu yeyote kujiajiri mwenyewe.

Aidha aliwashauri watendaji na maafisa hao kwenda kusoma ili kuongeza elimu itakayowasaidia kukabiliana na mabadiliko ya mageuzi katika Sekta ya Elimu nchini.

Aliwaahidi kuwa katika utendaji wake ataendelea kuwa karibu na kila mtendaji na kuhakikisha kila mtu anatekeleza wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii ili wapate haki zao kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.

“Katika mabadiliko haya kutakua na fursa mbili wapo Wanafunzi watakaosoma moja kwa moja masomo haya ya kawaida hadi Elimu ya Juu lakini wengine watasomea fani zao mfano masuala ya ujenzi,uvuvi,uimbaji,uchoraji,uchongaji wa samani,ushoni,ufundi,michezo na usanii wa aina zote kulinga na vipaji vyao,

Kwa upande wa Watendaji hao walisema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitendea kazi,Ofisi na huduma ya usafiri kwa watendaji hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.