Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 18-5-2023 na (kulia kwa Rais) Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalenzo Mhe. Juma Duni Haji na (kushoto kwa Rais) Kiongozi wa Chama Cha Act-Wazalendo Mhe. Zitto Zuberi Kabwe.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amekutana na Viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo ambao ni Mwenyekiti, Mhe. Juma Haji Duni, Makamu Mwenyekiti ambaye ni pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud na Mhe.Zitto Kabwe.

Pamoja na mambo mengine yanayohusu ustawi wa Zanzibar kisiasa na kijamii Viongozi hao wameafikiana kwamba ipangwe tarehe ya kuzindua rasmi kamati maalum itakayoundwa na wajumbe kutoka vyama vya CCM na ACT-Wazalendo ambavyo ndivyo vilivyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, kuanza kujadiliana  na baadae kupanga mpango wa utekelezaji wa ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa kufuatia Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliojadili maeneo mahsusi yanayoihusu Zanzibar. 

Kikao hicho kimefanyika Ikulu, Zanzibar 

🗓️18 Mei 2023

📍Ikulu , Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.