Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Nungwi na Jimbo la Kijini Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuimarisha chama.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamia dhana ya kukuza Uchumi wa Zanzibar kupitia Sekta ya Uchumi wa Buluu imetoa Boti zenye vifaa vya uvuvi kwa Wananchi ili waweze kujiajiri na kuzitumia katika kukuza Uchumi binafsi na Taifa kwa ujumla.
Ameeleza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi anaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo kwa kusimamia uwezeshaji wa wananchi kupitia shughuli mbali mbali.
Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha inaipatia ufumbuzi changamoto ya wanafunzi kutembea masafa marefu kwa ajili ya kufuata elimu kabla ya mwezi January 2024.
Aidha amefafanua kuwa Serikali imekusudia kuzitatua changamoto zote ikiwa ni pamoja na Elimu, Afya, Miundombinu ya Barabara na maji safi na salama.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar karibu itafunga Mkataba na kampuni kutoka Oman kwa ajili ya ujenzi wa miundombino ya maji safi na salama lengo ni kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Kaskazini wanapata huduma ya maji kwa uhakika.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu y CCM Taifa amefahamisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinathamini juhudi zinazofanywa na Mabalozi kuhakikisha wanakisimami Chama pamoja na kuimarisha uhai wa Chama kivitendo.
V Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa kaskazini kuwa huduma za Afya zitaendelea kuboreshwa ili wananchi waweze kupata huduma bora ambapo kwa sasa serikali imetenga Zaidi ya Shilingi Bilioni ishirini (20) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya nchini.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed ametilia mkazo suala la wanachama kulipa ada kwa wakati ili Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake zizidi kuimarika na kufikia maelekezo yaliyomo katka Ilani ya CCM.
Amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini unguja kuhakikisha wanawasimamia vijana wote waliofikisha umri wa miaka 18 waweze kutafuta kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi kitakachowasaidia katika shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpigia kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025 na kukiwezesha Chama Mapinduzi kuendelea kushikilia Dola.V ha Mapinduzi jambo ambalo litapelekea CCM kuendelea kushinda katika kila Chaguzi zote.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuitunza na kuilinda kwa nguvu zote Amani iliyopo Nchini sambamba na kuimarisha umoja na mshikamano, haki na usawa kwa watu wote.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Muhamed Mahmoud ameeleza kuwa Ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imelenga kuimarisha chama pamoja na kuonana na wananchi na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Amesema Mkoa wa Kaskazini Unguja umebahatika kupata miradi mingi inayowagusa moja kwa moja wananchi ikiwemo ujenzi wa Madarasa, vituo vya afya, huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Nao viongozi wa Majimbo hayo wameeleza faraja yao kwa maamuzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kujengea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Madarasa ambayo yamepunguza uhaba wa eneo la kusomea na uchimbaji wa Visima vya maji safi na salama.
Aidha wamemuhakikishia Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa wataendelea kuimarisha Chama hicho kwa kusimamia maelekezo aliyoyatoa ili Chama hicho kiendelee kukuwa zaidi.
Katika ziara hiyo Mhe. Hemed amepokea Taarifa za utekelezaji wa Majimbo hayo, ameweka Jiwe la msingi na kupanda Mti Tawi la CCM Kivunge ‘’B’’ pamoja na kushiriki ujenzi wa Tawi la CCM Jungu Kuu.
No comments:
Post a Comment