Habari za Punde

Mhe. Mazrui Aahidi Kuimarisha Huduma Kupitia Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na wadau wa   Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) wakati akifunga warsha ya msaada wa pili wa kiufundi wa kuanzishwa na utekelezaji wa bima ya afya kwa wote  (UHI), huko Ukumbi wa Mikutano Zura Maisara Mjini Unguja.

Na Rahma Khamis - Maelezo Zanzibar. 

Waziri wa Afya Zanzibar  Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara inaendelea kuchukuwa juhudi za kuhakikisha  Hospitali zote zinaanza kutoa huduma za Mfuko wa huduma ya Afya  kwa Wanannchi   ifikapo mwezi Octobar mwka huu.

Akifunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo watendaji wa Mfuko huo na wadau wa maendeleo huko katika Ukumbi wa Zura Maisara amesema kupitia huduma hiyo Wizara itahakikisha inatoa huduma bora za Afya kwa jamii na  kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi hao.


Aidha alieleza  kuwa Serikali itashirikiana na wadau wa maendeleo katika kufankisha upatikanaji wa huduma bora  za Afya kupitia Mfuko huo.


Hata hivyo amesema Serikali ina jukumu la kuhakikisha  kuwa wananchi wake wanakua  na afya bora ili kuweza kushiriki katika harakati za ujenzi wa Taifa.


Aidha Waziri amefahamisha kuwa  adhma ya  Serikali ya awamu ya nane chini uongozi wake Dkt Hussein Ali Mwinyi ni  kuhakikisha wananachi  wote  wanapata  huduma bora za afya bila ya kujali hali zao za kifedha.


“Muheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ,Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefanya ujasiri wa kuanzisha Mfuko wa huduma za Afya hivyo hakuna budi kumuunga mkono kwa hali na mali,”alikumbusha Waziri.


Ameongeza kuwa Zanzibar imechagua mpango wa Bima ya Afya kwa wote (Universal Health Insuarence Scheme) kama utaratibu wa ufadhili wa UHC ambao utagharamiwa kwa kodi ya jumla,michango ya wananchama na msaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.


Waziri alisema kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya fedha na Mipango itatoa msaada unaohitajika kuhakikisha mpango wa Universal Health Insuarence unafanikiwa na kutumika  nchini.


Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kujiunga katika Mfuko wa Hudma za Afya ili kupunguza usumbumbufu wanaoupata wakati wanapopata matatizo ya kiafya.

 

Nae Mwenyekiti wa Bodi  ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Mbarouk Omari Moh’d amesema mfuko huo ni mpya hivyo kunaweza kujitokeza changamoto mbalimbali hakuna budi kushirikiana na wadau wengineili kuweza kupata mipango na mawazo yao yatakayoweza kusaidia kuimarisha mfuko huo.

 

Aidha amefahamisha kuwa Serikali inategemea kupata fedha kutoka kwa wadau,wafadhili  pamoja  na wananchi wenyewe waliojiunga kuwezesha mfuko huo kuwa endelevu.

 

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya fedha za nje  Yussuf  Ibrahim Yussuf  amesema wamejipanga  kuhakikisha   fedha zinazotarajiwa kutumika katika mfuko huo zinapatikana kwa wakati uliopangwa.

                     

Aidha amesema ushirikiano  uliopo kati  ya Ujerumani na Zanzibar ni hatua moja  ya kuleta maendeleo katika kuinua na  kuimarisha maisha ya wazanzibar.

                                            

Warsha hiyo yenye lengo la kuimarisha Mfuko wa Hudma za Afya Zanzibar imeandaliwa na Mfuko wa Afya chini ya ufadhili wa  Wadau kutoka Ujerumani na Swizland.

Mkuu wa timu inayoongoza kitengo cha ufadhili wa Afya (GIZ) Nina Siegert akizungumza na Wadau wa Mfuko wa  huduma za Bima ya Afya wakati akiwasilisha matokeo ya Msaada wa pili wa Ujerumani kupitia GIZ juu ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa wote, huko Ukumbi wa Mikutano Zura Maisara Mjini Unguja. 


Kamishna Idara ya fedha za Nje kutoka Wizara ya fedha na mipango Zanizibar Yusuf  Ibrahim Yussuf akizungumza kuhusu matumizi ya Mfuko wa huduma za Afya wakati wa ufungaji wa warsha ya msaada wa pili wa kiufundi wa kuanzishwa na utekelezaji wa bima ya afya kwa wote Zanzibar (UHI),iliyowashirikisha wadau wa  Mfuko huo na kufanyika huko Ukumbi wa Mikutano Zura Maisara Mjini Unguja.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Mbarouk Omar akimkaribisha Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui kuzungumza na Wadau wa Mfuko wa Huduma za Afya klabla ya kufunga rasmi warsha ya msaada wa pili wa kiufundi wa kuanzishwa na utekelezaji wa bima ya afya kwa wote Zanzibar (UHI),iliyowashirikisha wadau wa  Mfuko Wa huo na kufanyika huko Ukumbi wa Mikutano Zura Maisara Mjini Unguja.
Mshauri wa Afya kutoka taasisi ya Mashirika ya Maendeleo SWISS Dkt. Yahya Ipuge akizungumza wakati wa  warsha ya msaada wa pili wa kiufundi wa kuanzishwa na utekelezaji wa bima ya afya kwa wote Zanzibar (UHI),iliyowashirikisha Waadau  wa Mfuko Wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) na kufanyika huko Ukumbi wa Mikutano Zura Maisara Mjini Unguja.

                     PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.