Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza na ujumbe wa shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kuwezesha maendeleo endeleovu kwa jamii (PACT) lenye makao makuu yake nchini Marekani. Ujumbe huo ulifika ofisini kwa makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 24.08. 2023 kwa kubadilishana mawazo na Mheshimiwa Makamu .
( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar.)
Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa
Zanzibar linalendelea kuwa changamoto kubwa inayohitaji jitihada za pamoja kwa mashirikiano kati serikali na
Wadau mbali mbali wa maendeleo katika kuandaa sera na mipango sahihi na
kuweka mikakati madhubuti ya utekelezaji katika kulikabili kwa ufanisi suala hilo.
Mhe. Othman
ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipofanya mazungunzo na Shirika
la Kimataifa lisilo la Serikali (PACT) , ambalo kwa kushirikiana na serikali
mbali mbali duniani linajishughulisha kuwezesha maendeleo endelevu kwa jamii, uimarishaji
wa Utawala bora na Demokrasia, na kuhudumia watu wenye changamoto na kuleta afua katika sekta za lishe ,elimu ,
uwezeshaji kiuchumi na utafutaji wa masoko.
Mhe. Makamu
amesema kwamba tatizo hilo ni kubwa na
limekuwa kuongezeka kwa kasi kila mwaka kwa kuwa vijana wengi wanaendelea
kukosa ajira na hivyo kuashiria kwamba jambao hilo linaweza kugeuka kwa ni
janga la baadae katika nchi jambo ambalo linahitaji jitihada kubwa katika
kuwawezesha vijana kwa kutumia rasilimali za ndani zilizopo hasa katika sekta
ya utalii.
Amefahamisha
kwamba Zanzibar hivi sasa ina hoteli za utalii zaidi mia sita, lakini mahitaji
makubwa ya hoteli hizo yanapatikana kutoka nje ya Zanzibar, na iwapo vijana nchini watawezeshwa ipasavyo sekta hiyo pekee
inaweza kuwa na uwezo na kutoa fursa kubwa za kutatua tatizo la ajira kwa
vijana nchini.
Aidha Mhe.
Othman amesema kwamba kupitia juhudi za pamoja kati ya serikali na Taasisi
zisizo za Serikali kama vile PACT inawezekana kuwawezesha vijana kujengewa
uwezo wa kujiajiri katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali zinazohitajika
katika soko la utalii jambo ambalo
litasaidia sana katika kuikabili changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
Amefahamisha
kwamba serikali haina uwezo wa kuwaajiri vijana wote waliopo na wanaomaliza
katika vyuo vikuu mbali mbali lakini kinachohitajika ni kuwepo mazingira sahihi
ya kuwawezesha katika sekta ya biashara ya utalii na ukarimu na kwamba bila
kuwawezesha vijana katika ajira taifa haliwezi kuwa na mabadiliko chanya
kimaendeleo.
Mhe. Othman
amesema kwamba vijana katika taifa
lolote wanapaswa kuandaliwa kuwa chachu ya mabadiliko ya kimaendeleo kwa kuangalia mahitaji yao muhimu kwa sekta
na maeneo tofauti kwa kuzingatia mahitaji ya
wakati wa sasa na wabaadae ili taifa liweze kupiga hatua Zaidi na kwa
haraka.
Akizungunzia
suala la athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi Mhe. Makamu amesema
kwamba Zanzibar kuna maeneo yapatayo kumi na nne (14), yamekumbwa na athari
hiyo ingawa juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa na serikali ikiwa ni pamoja na
upandaji wa mikoko lakini tatizo la athari hizo bado linaendea katika maeneo mbali mbali nchini.
Hata hivyo,
amesema kwamba serikali inaendelea na mikakati mbali ya kitaifa na kwamba hivi
karibuni itazindua mradi wa kuirejesha
Zanzibar kuwa ya kijani ambapo utekelezaji wake utahitaji ushiriki wa wadau
mbali mbali wa maendeleo katika kufikia ufanisi wa lengo lililokusudiwa la
kupunguza athari za mabadiliko ya taibia
nchi.
Akizungunzia
suala la vijana katika siasa Mhe. Othman
amesema kwamba wengi wao wanaingia katika siasa kwa matumaini ya kupata ajira
badala ya kufikiria kuwepo mabadiliko ya kimaendeleo jambo ambalo linabakia
kuwa ni changamoto kuwa kwa vijana.
Naye Rais wa
shirika hilo la PACT Dk. Caroline Anstey, amesema kwamba shirika hilo limekuwa
likifanya kazi kubwa na jamii katika nchi mbali mbali duniani katika kuweka
ustawi wa masuala ya afya kwa jamii pamoja na kusaidia kujenga uwelewa kwa
vijana katika masuala mbali mbali ikiwemo demokrasia, elimu na utawala bora.
Amesema kwamba
shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Marekani lipo tayari kufanya kazi na
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya kuwawezesha
vijana katika masuala, elimu , afya, ustawi wa jamii na demokrsia pamoja na
utawala bora na hivi sasa wanafanyakazi katika nchi 35 duniani kote.
Mwisho
Kitengo cha
Habari
Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Agosti 24, 2023
No comments:
Post a Comment