RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Kanisa la Anglikan Tanzania ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania Maimbo Mndolwa (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo,30-8-2023.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekua
ikihamasisha na kushajihisha watu wake kujitahidi kuzitumia vema fursa za lugha
ya Kiswahili na kuzifanyia kazi ya kutafsiri kwenye mataifa mbalimbali duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amehyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza
na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,
Maimbo Mndolwa aliefika kujitambulisha na ujumbe wake baada ya kuchaguliwa
kuongoza kanisa hilo mwezi Februari mwaka huu, kwa kipindi cha miaka mitano
ijayo.
Dk. Mwinyi alisema lugha ya Kiswahili imekua na fursa
nyingi duniani kutokana na kazi za ukalimali, hivyo aliwataka Wazanzibar na
Watanzania kwa ujumla kutumia fursa hizo kwa kuzichangamkia kwa wingi na
kuahidi ushirikiano baina ya kanisa na Serikali kuwashajihisha vijana
kuzichangamkia
“Sasa hivi tunapromote sana watu wetu kwenda kufanyakazi
za kutafsiri lugha ya Kiswahili, lakini wenzetu mataifa mengine wametuzidi, tunakazi
ya kufamuya tuko tayari kushirikiani na nyinyi kwaajili ya vijana wetu”
alieleza Rais Dk. Mwinyi.
Aidha, rais Dk. Mwinyi alimuahidi askofu huyo kuzungumza
na wahusika wa kamisheni ya Kiswahili ili kuona namna ya kuboresha ushirikiano
baina ya serikali na kanisa hilo.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekua na
uhusiano wa muda mrefu na kanisa hilo, hivyo aliutaka uongozi huo mpya
kuendeleza ushirikiano wao kwa Serikali hasa kwenye suala zima la kuendelea kuhubiri
amani, umoja na mshikamano kwani ni mambo muhimu kwa usatawi
na ujenzi wa Serikali na watu wake.
Akizungumzia masuala ya kuboresha Utalii Zanzibar, Rais
Dk. Mwinyi alilipongeza Kanisa La Anglikana kwa kazi kubwa wanayoifanya ya
kuwavutia watalii wengi sambamba na kupongeza hatua ya Kanisa hilo kuwaalika
watu wa kubwa duniani kuja Zanzibar hali itakayozidi kuitangaza Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla kimataifa pamoja na kukuza sekta ya utalii.
Pia, Rais Dk. Mwinyi alilipongeza Kanisa hilo kwa juhudi
zao za kupinga harakati za biashara ya kuuza binaadamu ambayo imeshamiri sana
duniani sambamba na kumueleza Askofu Maiombo kwamba Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar inaungamkono hatua hiyo, wadau na wanaharakati wote wanaopinga
udhalimu huo.
Rais Dk. Mwinyi aliupongeza na kuukariribisha uongozi wa
Kanisa hilo na kuueleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekua na ushirikiano
mzuri na kanisa hilo hivyo aliomba kuendeleza uhusiano uliopo kwa manufaa ya
wanaumini wao na Serikali kwa ujumla
Naye Askofu Maimbo Mndolwa alimpongeza Rais wa Zanzibar
kwa maendeleo makubwa aliyoyafanikisha kipindi kifupi cha uongozi wake.
Askofu Maimbo alimueleza Rais Dk. Mwinyi mpango wa Kanisa
hilo kutumia historia ya biashara ya utumwa Zanzibar, kama ni fursa adhimu ya
kukuza utalii kwa Zanzibar kupitia kanisa hilo ambalo limekua kivutio kikubwa
kwa watalii wengi wanaofika nchini.
Alimuahidi Rais Dk. Mwinyi kwamba kanisa linampamgpo wa
kuwaalika mataifa makubwa akiwemo Gavana mkuu wa Ujerumani kuja Zanzibar kwani
taifa hilo liliacha athari na histotia kubwa ya biashara ya utumwa Zanzibar
pamoja na mataifa mengine ya Mashariki ya mbali kwa lengo la kuitangaza
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa njia za utalii pia kuweka mkazo kwenye
sekta hiyo.
Sambamba na kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kuangalia uwezekano wa kuimarisha kiiutalii maendeneo ya kanisa hilo kwani
limekua kivutia kikubwa kwa wageni na kuiomba Serikali kuangalia namna ya kufunga
mashine za kudhibiti mapato yanayotokana na utalii ili kuzuia mianya ya kodi za
Serikali zisipotee mikononi mwa wasiohusika.
Akizungumzia umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwenye anga za
Kimataifa Askofu Maimbo alimomba Rais Dk. Mwinyi ushirikiano baina ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kamisheni ya Kiswahili kushirikiana kuwaandaa vijana
ili wakawe wakalimali wazuri kimataifa kwani nafasi nyingi nimechukuliwana
Wakenya na Wakongo.
Alieleza Tanzania ina fasaha nzuri ya lugha ya kiswahilli
hivyo aliziomba Serikali za SMZ na SMT kwa ushirikkiano wa Kanisa la Anglikana
Tanzania kuitumia fursa hiyo kwa watanzania kunufaika.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Kanisa la Anglikan Tanzania ukiongozwa na
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania Maimbo Mndolwa (kulia kwa Rais)
mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
leo,30-8-2023.
No comments:
Post a Comment