RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali
ya China kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar
kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.
Dk. Mwinyi ametoa
shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipowakabidhi vyeti na medali timu ya madaktari
32 kutoka China waliohudumu kwenye hospitali za Zanzibar kwa kipindi cha mwaka
mmoja na kuwaaga baada ya kumaliza muda wao nchini.
Rais Dk. Mwinyi amesema,
Zanzibar imenufaika na fursa nyingi kutoka China kupitia sekta mbalimbali za maendeleo
ikiwemo Afya hususan kupokea timu za madaktari bingwa wanaofika nchini
kubadilishana uzoefu na wazawa hali aliyoieleza imeimarisha uhusiano mwema
uliopo baina yao pamoja na kujifunza uzoefu wa masuala mbalimbali ya afya.
Dk. Mwinyi alieleza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imeendeleza maeneo mengi ya afya kwa kujenga hospitali zenye vifaa
tiba vya kisasa, kuboresha miundombinu na kuongeza hospitali za wilaya na mikoa
pamoja na kuifanyia matenegezo makubwa hospitali ya Mnazi Mmoja.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameshukuru kazi kubwa
iliyofanywa na timu hiyo ya madaktari 32 kipindi chote walichohudumu Zanzibar
na kusema Serikali ilnajivunia sana kuwepo kwao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri wa Afya Nassor
Ahmed Mazrui alisema aliishukuru timu ya madaktari hao nakueleza ushirikiano
uliopo baina ya China na Zanzibar umedumu kwa miaka 60 sasa.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Amour Suleiman
Mohammed alisema timu hiyo ya madaktari bingwa kutoka China iliwasili nchini
Septemba 26 mwaka 2022 na Septemba 26 mwaka huu inatarajiwa kurejea kwao.
Alisema timu hiyo ilitoa msaada wa kitabibu kwa
wananchi wa Unguja na Pemba kwa magonjwa ya macho, meno, mkojo, figo, huduma za
X- ray, pia ilifanya upasuaji kwa
wagonjwa zaidi ya 50 kwa maradhi tofauti.
Kiongozi mkuu wa timu ya madaktari hao 32 , Dk. Zhao
Xiaojun alishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano ilioutoa
kipindi chote na kueleza Zanzibar ni visiwa vyenye upendo, amani na mshikamano
kwa wenyeji na wageni.
Alishukuru pia ushirikianao kwa wenyeji wao
madaktari wa Zanziba na kueleza upendo wao ulikakisi maudhui ya uwepo wao
nchini
“Kamwe hatutasahau uzuri na haiba ya mandhari ya
visiwa vya Zanzibar vilivyopambwa kwa maumbile ya anga la buluu, fukwe nyeupe,
uzuri wa mwanga wajua linapochomoza, kijani cha minazi na ukarimu wa watu wake,
yote haya tutayakosa baada ya kuondoka Zanzibar” kwa hisia alisifia
Hata hivyo, timu ya
madaktari hao ilimuahidi Dk. Mwinyi kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao.
No comments:
Post a Comment