Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Awasili Wilaya Geita

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ameondoka Zanzibar na kuwasili Mkoani Geita Wilaya ya Chato akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufungaji wa Maonesho ya Sita (6) ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini  yatakaofanyika kesho  30. 09.2023 katika viwanja vya kituo cha Uwekezaji Cha Bomba mbili Mkoani Geita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia Wananchi wa Geita alipowasili Uwanja wa Ndege Geita leo.

Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR)

Trh.29.09.2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.