RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amalitaka Baraza la
Maulidi Zanzibar kuendelea kusimamia na kutoa maelekezo na miongozo mizuri ya
usomwaji wa maulidi nchini kwa kwani kwa kiasi kikubwa maadili yamekiukwa kwa miaka
ya karibuni.
Ahaj Dk. Mwinyi aliyasema
hayo alipozungumza kwenye hafla ya Baraza la Maulid Zanzibar, Ukumbi wa
Sheikh Idriss Abdulwakil, Mkoa wa Mjini Magharibi
Alisema, Baraza la
Maulid Zanzibar litasaidi kurejesha misingi sahihi ya usomwaji bora wa Maulid
kwa kuwatumia wanazuoni wa ndani na nje ya nchi.
Alhaj Dk. Mwini
alieleza, sherehe za mazazi ya Mtume S.A.W zinafaida kiuchumi na jamii mbali na
kukuza umoja wa jamii na maeneo kwa watu kualikana kutoka maeneo mablimbali
hali iliyochangia kwa kiasai kikubwa kukuza mahusiano na biashara.
Alisema, historia ya
Mwambao wa Afika Mashariki imedhihirisha kukua kwa mahusiano yaliyochangiwa
kuimarika kwa watu wa maeneo tofauti kualikana mihadhara ya maulidi jambo lililochangia
kukuza ushirikiano na kuanzishwa biashamba mbalimbali baina yao na manufaa
makubwa yalipatikana kwa jamii kubasilishana mila na silka njema.
Alisema, Zanzibar
kuliwahi kuishi masheikh wakubwa waliotokana na mialiko ya maulidi kutoka
maeneo mbalimbali ya mwambao na wengine wakitokea nchi za Oman, Yemen, Komoro
ambao walitoa mchango mkubwa kwa Zanzibar.
Pia, alieleza usomwaji
wa maulidi unakwenda sambamba na mazazi ya Mtume S.A.W kama
yalivyofanywa na wanazuoni waliopita kwa kuzingatia maadili ya kiislam
Alhaj Dk. Mwinyi
aliipongeza Ofisi ya mufti Zanzibar kwa kusimamia vyema kusimiamia na kuratibu
shughuli mbalimbali za dini na kusimamia maadili ya vijana.
Vile vile alieleza
Maratajio ya Serikali kwa Baraza hilo la Maulid litasaidia ni kuwaunganisha
waumini wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kuisoma vizuri Sira na
mwenendo mzuri wa Mtume S.AW ili kujenga misingi bora ya kuendesha shughuli za
Maulid.
Akizungumza kwenye hafla
hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Maulidi ambae pia ni Kaadhi Mkuu wa
Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali aliitaka jamii kuendelea kumshiba Mtume (SAW)
kwenye maisha yao yote kwa kufuata yote maarisho yake na kuyaacha makatazo yake
ili kuepukana na matendo maovu yakiwemo udhalilishaji na ya upotevu wa maadili.
Naye, Sheikh Khalid
Mfaume, Katibu wa Ofisi ya Mufti aliitaka jamii kuendelea kusheherekea Mauli ya
kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW kwa nidhamu, heshma na mila na silha za dini ya
Kiislam kwa kuepuka michanganyiko na miingiliano ya waumini wananwake na wanaume
kwenye eneo moja.
Aidha alisifu
kuimarika kwa shughuli za dini ya Kiislam Zanzibar kwa kuendelea kupata baraka
za kiongozi wa mkuu wan chi, Alhaj Rais Dk. Hussein Mwinyi ambae alisifu
jitihada zake za kushirikia na waumini mbalimbali wa dini hiyo kwa nyakati
tofauti kwenye maeneo yote ya Zanzibar.
Alisema Alhaj Dk.
Mwinyi amekua kinara wa kuhimiza ibada kwa kujumuika nao kwenye Ibada za sala
misikitini, kusali nao pamoja Taraweikh kipindi cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani, Kushirikiana nao vyema kwenye sherehe za mwaka mpya wa Kiislam 1445
H pamaja na sherehe za mazazi ya Mtume (S.A.W) yaliyofanyija juzi kwenye
viwanja vya Maishara.
Kwaupande wake Sheikh
Muhamad Hassan Al Habsy kutoka Yemen aliiusia jamii ya Wazanzibari kuendelea
kuishi na matengo ya Mtume S.A.W kwa kutii na kumtukuza kwani uhakika wa dini
na matendo yake ni kutoka kwa Allah (S.W).
Shughuli hiyo ilihudhuriwa
na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Alhaj Haroun Ali Suleiman,
Waziri wa Ofisini ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Harusi Said, Katibu
Mkuu kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandis Zena Ahmed Suleiman,
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi, Idriss Kitwana Mustafa na viongozi wengine.
IDARA YA
MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment