Habari za Punde

Tangazo la Ajira

 


AFISI YA RAIS, KAZI , UCHUMI NA UWEKEZAJI  KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ABU DHABI, UMOJA WA FALME ZA KIARABU UNATANGAZA NAFASI ZA KAZI KATIKA HOTELI YA ST. REGIS AL MOUJ MASCAT.


NAFASI HIZO NI:

1. Vyakula na Vinywaji (Food and Baverage)

2. Mapokezi (Front Office)

3. Usafi na Upishi (House Keeping and Culinary)

SIFA ZA MUOMBAJI:

Muombaji anatakiwa kuwa na vyeti vya Taaluma Husika.

Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiengereza

Waombaji wote wanatakiwa kufanya usaili na kutuma maombi yao kupitia email: patricia.lorentehidalgo@marriott.com

Usaili unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu na Jumanne ya tarehe 11 na 12/09/2023, saa 4:00 asubuhi mpka saa 11:00 jioni katika Hoteli ya Serena- Zanzibar.

TANBIHI:

Waombaji wote wanatakiwa kuchukua CV zao pamoja na tiketi za uthibitisho wa usajili katika Siku ya Usaili (interview).

Maombi ya usaili huo ni bure na hakuna malipo yoyote.

Kwa Maelezo fika Afisi Ya Rais Kazi Uchumi Na Uwekezaji iliyopo Mwanakwerekwe   katika Idara ya Ajira.


SHIME VIJANA KUJITOKEZA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

 AFISI YA RAIS KAZI UCHUMI NA UWEKEZAJI – ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.