Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na Ujumbe wa Jeshi la Nchi Kavu la India Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akiwakaribisha Viongozi wa Ujumbe wa Jeshi la Nchi Kavu la India wakiongozwa na Jenerali Manoj Pande  walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo.

Dk. Mwinyi alizungumza na Mkuu wa Jeshi kutoka India, Jeneral Manoj Pande na ujumbe wake wa watu watano waliofika Ikulu, Zanzibar kumtembelea.

Katika Mazungumzo yao Rais Dk. Mwinyi aliueleza ujumbe huo uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na India na kushirikiana kwenye masuala mbali mabli ikiwemo ulinzi na usalama, masuala ya uchumi na huduma za jamii ikiwemo elimu, maji na teknolojia.

Alisema Ubalozi Mdogo wa India uliopo Zanzibar umekua na ushirikiano mzuri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kushirikiana kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoletwa Zanzibar na nchi hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa   Jeshi la Nchi Kavu kutoka nchini India (kulia kwa Rais) wakiongozwa na Jenerali Manoj Pande  walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa   Jeshi  la Nchi Kavu  kutoka nchini India wakiongozwa na Jenerali Manoj Pande (wa pili kulia)  walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akipokea  zawadi ya kutoka kwa  Jenerali Manoj Pande Kiongozi wa Ujumbe wa Kijeshi wa Jeshi la Nchi Kavu kutoka Nchini India walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo baada ya mazungumzo na ujumbe huo.[Picha na Ikulu] 04/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar, Jenerali Manoj Pande Kiongozi wa Ujumbe wa Kijeshi wa Jeshi la Nchi Kavu kutoka Nchini India walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu] 04/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akibadilishana mawazo na  Jenerali Manoj Pande , Kiongozi wa Ujumbe wa Kijeshi wa jeshi la Nchi Kavu kutoka Nchini India walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo baada ya mazungumzo na ujumbe huo.
[Picha na Ikulu] 04/10/2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.