RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Salmin Amour Juma.
Ndg.Amini Salmini Amour, alipowasili katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo
Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa na
kuhudhuria shughuli ya Maulid ya Mfungo Sita ya Kidombo na kisomo cha Hitma na Dua
ya kuwaombea Wazee, iliyofanyika baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa leo
6-10-2023. na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub
Mohammed Mahmoud
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, wakiwa katika
Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya Ibada ya
Sala ya Ijumaa na kuhudhuria Maulidi ya Mfungo Sita ya Kidombo na kisomo cha
Hitma na Dua ya kuwaombea Wazee, iliyofanyika baada ya kumaliza kwa Sala ya
Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo leo 6-10-2023.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Kidombo katika kisomo cha hitma na dua ya
kuwaombea Wazee, baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika
Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo, na kuhudhuria Maulidi ya Mfungo Sita hufanyika
kila mwaka Kijijini hapo na (kulia kwa Rais) Ndg. Amini Salmini Amour na
(kushoto kwa Rais) Mzee wa Kijiji cha Kidombo Sheikh.Salum Juma, wakisoma hitma
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akijumuika na Wananchi wa Kijij cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja katika
kisomo cha Hitma na dua ya kuwaombea Wazee wa Kidombo, baada ya kumalizika kwa
Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo leo
6-10-2023, na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj
Dk.Salmini Amour Juma Ndg.Amini Salimini Amour.Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Mzee wa Kijiji cha
Kidombo Sheikh. Salum Juma,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, Rais
Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Waumini mbali mbali wakiwa katika kisomo cha Khitma na Dua maalum sambamba na Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja,yaliyohudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa akiwa Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani).
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Kidombo, akiitikia dua ya kuhitimisha
hitma ya kuwaombea Wazee wa Kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja
ikisomwa na Sheikh. Salum Juma (kushoto kwa Rais) na Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh.Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Ndg. Amini Salmini Amour na Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, iliyofanyika katika
Msikiti wa Mkuu wa Ijumaa Kidombo leo 6-10-2023
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiongozana na Viongozi wa Serikali wakielekea nyumbani kwa Rais Mstaafu wa
Zanzibar Alhajj Dk.Salmini Amour Juma kwa ajili ya kumsalimia baada ya
kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo cha Hitma na Dua ya kuwaombea
Wazee wa Kijiji cha Kidombo, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo
Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 6-10-2023, (kushoto kwa Rais) Ndg. Amini Salmini
Amour na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mohmoud na (kulia
kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
RAIS
Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dk.Salmini Amour Juma akijumuika na Viongozi wakuu
wa Serikali katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh
Omar Kabi (hayupo pichani) walipofika nyumbani kwake Kidombo kwa ajili ya
kumsalimia baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma na dua ya kuwaombea Wazee
iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
6-10-2023, na (kulia kwa Alhajj Salmini) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.
Ayoub Mohammed Mahmuod na (kushoto kwa Alhajj Salmini ) Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj
Dk.Ali Mohamed Shein
RAIS
wa Zanzibar na Mwemyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini
Unguja leo 6-10-2023, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo
cha Hitma na Dua ya kuwaombea Wazee wa wa Kidombo, iliyofanyika katika Msikiti
Mkuu wa Ijumaa Kidombo.
WANANCHI
wa Kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsalimia Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati
akiwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo cha
Hitma na Dua ya kuwaombea Wazee wa Kidombo, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa
Ijumaa Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 6-10-2023.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwasalimia Watoto wa Kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya
kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo cha Hitma na Dua ya kuwaombea
Wazee wa Kijiji hicho iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kidombo leo
6-10-2023.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa Kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini
Unguja, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo cha Hitma na
Dua ya kuwaombea Wazee wa Kijiji hicho iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa
Ijumaa Kidombo leo 6-10-2023
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, baada
ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na kisomo cha Hitma na Dua ya
kuwaombea Wazee wa Kijiji Kidombo iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa
Kidombo leo 6-10-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Kiislamu kwenye Ibada ya Sala ya Ijumaa, huko Mkwajuni Kidombo, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mbali na ibada hiyo, Alhaj Dk. Mwinyi pia ameshiriki kwenye hitma na du’a maalum zilizosomwa baada ya ibada ya Sala ya Ijumaa kwa kuwaombea viongozi waliopo serikalini, wastaafu, masheikh na wazee walio hai na waliofariki dunia, ndani na nje ya Kijiji hicho.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akiwemo Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Marais wastaafu, Alhaj Dk. Salmini Amour Juma na Alhaj Dk. Ali Muhamed Shein, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Saleh Omar Kaab, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mahmoud na viongozi wengine wa dini.
Alhaj Dk. Mwinyi pia alipata wasaa wa kusalimiana na wananchi wa Mkoa huo wa Kaskazini Unguja na kuwatakia kheir.
Akikhutubu kabla ya sala ya Ijumaa Khatib Sheikh, Abdulkarim Said Abdulla kutoka Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, aliwasihi wananchi kuendelea kuwaombea du’a njema viongozi wa Serikali kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuitumikia nchi na harakati zao za kuendelea kuiletea maendeleo.
Pia aliwaomba viongozi hao kuwaomba viongozi hao kuendelea kuwatumikia, kuwapenda na kuwahurumia raia.
Pia, Sheikh Abdulkarim aliikumbusha jamii ya Kiislam juu ya suala zima la kumpenda Mtume Muhammad (SAW) kwa kufuata mema yote na kuachana na mabaya aliyoyakataza
Ibada hizo zilitekelezwa kufuaftia mwaliko kwa viongozi wa Kitaifa unaotolewa kila mwaka na Rais Mstaafu, Alhaj Dk. Salmin Amour Juma, ulioambatana na sherehe za usomwaji wa Maulid ya kumswalia Mtume Muhammad (SAW), kiijijini hapo.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment