
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kuhitimisha Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.
Tamasha la Ngoma za Asili
lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival ” ni kichocheo kikubwa
katika kukuza ajira na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameyasema hayo wakati akihitimisha tamasha hilo
lililoambatana na mbio za “Tulia Marathon” lililofanyika leo Septemba 30,2023
jijini Mbeya.
“Tamasha hili ni moja ya zao
jipya la utalii wa utamaduni ambalo limekuwa ni chombo muhimu cha kukuza na
kuhifadhi utamaduni wa Tanzania kupitia Ngoma za Asili” Mhe. Kairuki
amesisitiza.
Amefafanua kuwa tamasha hilo
limekuwa na manufaa makubwa kwa jamii na wasanii wa Ngoma za Asili kwa kusaidia
kukuza na kutambulisha tamaduni za Tanzania, kutoa ajira pamoja na kuchochea ukuaji wa utalii katika
jiji hilo kwa kuwavutia wageni kutoka
ndani na nje ya nchi.
Aidha, amesema Tamasha hilo ni
mwendelezo wa jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na utekelezaji wa mikakati ya Serikali
ya kuongeza mazao ya utalii.
Amewataka wadau na washiriki wa
tamasha hilo kutumia fursa ya uwepo wa tamasha hilo kuwekeza katika shughuli mbalimbali za utalii
kama vile wakala wa biashara za utalii, kujenga kambi za kulala wageni, kujenga
hoteli, kumbi za mikutano na maeneo ya michezo mbalimbali mkoani Mbeya.
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameiomba Serikali kuunga mkono tamasha
hilo kwa lengo la kuhakikisha utalii unakua katika ukanda wa Nyanda za juu
Kusini.
Tamasha la Ngoma za Asili
lililoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, lilianza tarehe 28 hadi 30 Septemba, 2023 lengo ikiwa
ni kuenzi asili na utamaduni wa Mtanzania pamoja na kukuza zao jipya la Utalii
wa Utamaduni hasa katika Nyanda za Juu Kusini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihitimisha Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika Septemba 30,2023 jijini Mbeya.
Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakifuatilia matukio katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika
Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika
Meza kuu ikipiga makofi kuashiria kufurahia ngoma za asili zilizokuwa zikitoa burudani katika jukwaa kuu kwenye Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya. Wa tatu kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na viongozi wa Chama na Machifu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)akiteta jambo na Mtoto mchezaji wa ngoma za asili kutoka kikundi cha ngoma za asili cha Utandawazi, Katondo Kebera (kushoto)katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) wakicheza ngoma za asili katika katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimuonyesha vyakula vya kiutamaduni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wa pili kushoto) ,vilivyopikwa katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi namba moja wa vyakula vya kiutamaduni katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ORYX, Araman Benoit.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa kikundi cha ngoma za asili cha ekigoma katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment