Afisa kutoka Taasisi ya Mifugo Wizara ya Kilimo Dk.Othman Juma akiwasilisha mada ya kanuni ya nyama wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwelewa wadau wa nyama yaliyofanyika Ofisi za ZFDA Mombasa Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Na Fauzia Mussa ,Maelezo
Mkurugenzi Idara ya udhibiti usalama wa Chakula Dkt.Khamis Ali Omar kutoka Wakala wa Chakula ,Dawa na Vipodozi, ZFDA, amewataka wamiliki wa machinjio kudumisha usafi katika machinio yao, ili kuhakikisha machinjio hayo yanakua salama.
Akizungumza na wadau hao wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwelewa juu ya kanuni ya nyama amesema kufanya hivyo kutapelekea bidhaa inayopatikana hapo kuwa salama kwa mtumiaji.
Amesema kabla ya mafunzo hayo ZFDA ilifanya ukaguzi na kugundua mapungufu mbalimbali katika machinjio, ambayo kama wakala walitoa mapendekezo juu ya namna ya kuyafanyia kazi.
Amefahamisha kuwa baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo ZFDA itaanza kuchukua hatua ya kuyafungia machinjio yote yanayoenda kinyume na kanuni na sheria zao hadi pale yatakapokidhi vigezo.
Akielezea kuhusu muongozo wa chinjio Mkaguzi wa Chakula ZFDA Mwajuma Kombo Ali alisema ili machinjio yawe salama na kukubalika ni lazima yazingatie vigezo ambavyo vimo kisheria ikiwemo kuwa na sehemu ya maji safi na salama,mitaro, sehemu ya kuewkea maji na kutenganisha sehemu ya kukaguliwa na kuchinjia mnyama .
Akiwasilisha mada ya kanuni za nyama Ofisa kutoka Taasisi ya Mifugo ya Wizara ya Kilimo Dk.Othman Juma amesema kanuni ya nyama ya mwaka 2015 inasisitiza kuzingatia haki za mnyama, hivyo mmiliki anaweza kufungiwa endapo itagundulika hazingatii haki za mnyama huyo akiwa hai.
“kuna wachinjaji wanawakata viungo kabla ya kuwachinja hii sio haki ya mnyama”alifahamisha
Nao Washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kubadilika kwa kuayafanyia kazi mafunzo hayo ili kulinda afya za watumiaji.
Hata hivyo wameishauri ZFDA kuweka wakaguzi wao katika masoko ili kuendelea kudhibiti uchinjaji holela.
“sokoni kule ndio mtajua kama kana watu wanachinja kienyeji mana nyama itaingia sokoni bila ya muhuri”walisisitiza
Mafunzo hayo ya siku moja yaliwashiriksha wamiliki na watendaji wa machinjo mbalimbali ya binsafsi na Serikali ikiwemo Chinjio la Donge Muwanda,Mahonda,Kinyasini,
No comments:
Post a Comment