Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Atembelea Maonesho Kabla ya Kufungua Wiki ya Huduma za Fedha

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kisongo Arusha ambako alifungua  Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo, Novemba 22, 2023. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela na wa tatu kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajasiriamali wakati alipotembelea banda la maonesho la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023. Kulia  kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meneja Huduma   kwa Jamii wa Benki ya Watu wa Zanzibar, (PBZ), Muzne Hamed Mohammed  wakati alipotembelea banda la maonesho la benki hiyo kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, wa tatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako. Wa pili kulia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Hosea Kashimba wakati alipotembelea banda la maonesho la mfuko huo kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anjela Mziray (kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho la mfuko huo kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha , Novemba 22, 2023. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa, Joyce Ndalichako (kulia ),  Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi takati alipotembelea banda la maonesho la NBC kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya  Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Novemba 22, 2023.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.