Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ameondoka Ncheni Akielekea Nchini Qatar Kuhudhuria Mkutano wa Kongamano la Uchumi Doha

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mama Sharifa Omar Halfan na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa  na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, wakati akielekea Doha Nchini Qatar leo 8-12-2023, kuhudhuria Mkutano wa Kongamano la Uchumi linalofanyika Doha Nchini Qatar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana  na kuagana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar alipowasili katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Doha Nchini Qatar leo 8-12-2023, kuhudhuria Mkutano wa Kongamano la Uchumi linalofanyika Jijini Doha Nchini Qatar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Mama Mariam Mwinyi, akiwa katika  ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akizungumza na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkewe Mama Sharifa Omar Halfan, akielekea Jijini Doha Nchini Qatar kuhudhuria Mkutano wa Kongamano la Uchumi linalofanyika Jijini Doha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi mbalimbali wa Serikali, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Qatar,kuhudhuria Mkutano wa Kongamano la Uchumi linalofanyika Jijini Doha Qatar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.