Habari za Punde

Wazee Watakiwa Kufanya Mazoezi Ili Kujikinga na Maradhi Yasioambukiza - Bi. Salama

Na Rahma Khamis Maelezo, 30/12/2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazee na Wastaafu Zanzibar (JUWAZA) Bi.Salama Kombo Ahmed amewataka Wazee kuendelea kufanya mazoezi ili kujikinga na maradhi yasioambukiza.

 

Wito huo ameutoa wakati wa Sherehe za Wazee wa Shehia ya Magomeni na Mea Wilaya ya Mjini, ikiwa ni shamrashamra za kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Amesema mazoezi yanasaidia kujikinga na mambo mbalimbali ikiwemo maradhi nyemelezi hivyo ni vyema kufanya mazoezi ili kuepukana nayo.

 

Ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa Jumuiya hiyo ni kuibua changamoto, kujadili na kuweka mikakati itakayoweza kuwasaidia Wazee kuepukana na matatizo yanayowakabili kama vile maradhi, kutengwa na jamii.

 

Amefahamisha kuwa Wazee na Wastafu wanahitaji kupatiwa huduma bora kama vile matunzo na huduma za Afya kwani baadhi yao wamekuwa wakizikosa mara baada ya kustafu.

 

Amefafanua kuwa Jumuiya hiyo ina kazi ya kushughlikia haki za Wazee,kuunda na kusimamia Mabaraza yao ili waweze kupaza sauti zao na kusikika kupitia Mabaraza ya Shehia na Wilaya.

 

"Tumeamua kuunda Mabaraza ya Wazee katika kila Shehia na Wilaya ili tuwatoe Wazee ndani na kwenda kujishughulisha na kufanya Mazoezi kwani kufanya hivo itawasaidia Wazee hao kuacha kujifungia majumbani," alifahamisha Katibu Mkuu huyo.

 

Aidha amesema Jumuiya imebaini kuwa, baadhi ya Wazee wanapata Maradhi yasiyoambukiza hivyo wameanzisha Mradi wa kuwasomesha Wazee masuala hayo ili waweze kupata uelewa wa kutosha na kuweza kujikinga na Maradhi hayo.

 

"Wazee fanyeni mazoezi sisi Jumuiya tupo kwa kushirikiana na Serikali, tutakusaidieni kwa kila hatua" alifafanua

 

Amewaomba Wazee waliyotimiza miaka 50 kufika Hospitali kupima afya zao hasa Tenzi dume kwa Wanaume.

 

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Mjini Kondo Ameir Zaidani amewataka Wazee hao kutumia vyakula bora na kufanya Mazoezi ili kuimarisha afya zao.

 

Amesema Serikali inachukuwa juhudi za kutoa Misada kwa Wazee kwa azma ya kuwawezesha kufikia malengo yaliopangwa na Serikali kustawisha jamii ikiwemo Wazee.

 

 Nao Wazee wa Jimbo la Mgomeni wameahidi kufanya mazoezi kwa bidii ili kupata kuimarisha afya zao na kushiriki katika harakati mbalimbali za kimaisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.