Habari za Punde

Tigo Zantel Yapiganga Kuhakikisha Inaendelea Kutoa Huduma Bora Kwa Wazanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi  wa Kanda wa kampuni ya Simu ya Tigo Zantel Ndg,Aziz Said Ali wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho katika hafla ya ufunguzi wa Eneo la Maonesho ya Biashara na Tamasha la 10 la Biashara Zanzibar,Nyamanzi Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo ni katika maadhimisho ya shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (katikati)  Mke wa Rais  Mama Mariam Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata  maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  wa Kanda wa kampuni ya Simu ya Tigo  Zantel Ndg,Aziz Said Ali wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho katika hafla ya ufunguzi wa Eneo la Maonesho ya Biashara na Tamasha la 10 la Biashara Zanzibar,Nyamanzi Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo ni katika maadhimisho ya shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Omar Said Shaaban.

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Zantel ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa Maonyesho hayo ambapo Mkurugenzi wa Tigo Zantel Zanzibar Azizi Said amesema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wazanzibar na kuomba ruhusa ya kuunganisha mifumo ya malipo kwa kampuni mbalimbali ambazo zinatekeleza miradi ya ujenzi hapa Zanzibar pamoja na kuongeza wigo katika malipo ya ndani ya serikali

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.