Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Februari 15, 2024 amechukua Fomu ya Kugombea Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Ngazi ya Taifa.
Mheshimiwa Othman amepokea Fomu hiyo ambayo imedhaminiwa na kukabidhiwa kwake kutoka kwa Wenyeviti na Makatibu wa ACT-Wazalendo wa Mikoa 27 ya Kichama, ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Hafla hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Kigoma, Kiiza Mayeye imefanyika katika Ofisi kuu ya Chama hicho, Vuga Mjini Unguja.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Februari 15, 2024.
No comments:
Post a Comment