Habari za Punde

Zanzibar Yachaguliwa Kuwa Mwenyeji wa Michuano ya Chalenji Senior Cup

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita, akimezungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake iliyopo Migombani Zanzibar.

Katika mkutano huo, Mhe. Waziri Ametangaza kuwa  Zanzibar imebahatika kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Challenge Senior Cup mwaka huu ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu Viwanja vya New Amani Complex.

Aidha Amempongeza na kumshukuru kwa dhati Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi kwa Maamuzi yake ya kijasiri na Upendo kwa Maendeleo yenye kasi hususan katika sekta ya michezo yalio pelekea Zanzibar kuteuliwa kua mwenyeji wa mashindano haya.

Pia amesisitiza umuhimu wa maandalizi bora kwa timu za Taifa za ndani na nje ya nchi zitakazoshiriki. 

Aidha, ameonyesha azma ya kuitetea tasnia ya michezo kwa kuirejesha kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde (SAZI) ili kusaidia katika maandalizii hayo 

Wajumbe walio teuliwa na Mhe. Waziri Tabia ni pamoja na:

1. Mheshimiwa Ayoub Mohammed Mahmoud (Mwenyekiti)

2. Ndugu Said Kassim Marine (Katibu)

3. Mheshimiwa Nassor Ali Salim Jazira

4. Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza

5. Mheshimiwa Fatma Ramadhan Mandoba

6. Ndugu Arafat Ally Haji

7. Ndugu Mwalimu Ali Mwalimu

8. Ndugu Naima Said Shaame

9. Ndugu Ramadhan A. Bukini

10. Mheshimiwa Abulghafar Idrissa Juma

Mhe. Waziri Mwita ameonyesha imani yake kwa kamati hii na ana matarajio makubwa kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kufanikisha mashindano haya makubwa. 

ChallengeSeniorCup2024 #Zanzibar 

Imetolewa na kitengo cha habari  WHVUM

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.