Habari za Punde

Maadhimisho ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa Zanzibar na Kuwaombea Dua Yaendelea

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaabani Ali Othman akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika hafla ya dua kumuombea Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mstaafu Khamis Darweshi Mdingo na Kanali Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omari Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaabani Ali Othman katikati akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika hafla ya dua kumuombea Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mstaafu Khamis Darweshi Mdingo na Kanali Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omari Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaabani Ali Othman akizungumza  na Wananchi na Wanafamilia baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mstaafu Khamis Darweshi Mdingo na Kanali Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omari Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Kiongozi wa Familia Darweshi Kamis Darweshi akitoa neno la Shukurani baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mstaafu Khamis Darweshi Mdingo na Kanali Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omari Ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro Shirazi pamoja na siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume,hafla iliofanyika Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.02/04/2024.

Na.Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Uchumi wa Buluu  na Uvuvi Mhe. Shaabani Ali Othman  amewasihi wananchi walioondokewa na wazazi wao kuendelea kushikamana ili kuepusha migogoro katika familia.

Ameyasema hayo huko Kiembesamaki  Wilaya ya Magharibi ‘B’ katika dua maalumu ya kumuombea  aliyekuwa Kamishna  Msaidizi Mstaafu wa Polisi Zanzibar Marehemu Khamis Daruweshi ikiwa ni muendelezo wa wiki ya kuwaenzi viongozi wa kitaifa.

Ziara ya kutembelea makaburi ya Viongozi  wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuwa dua ni chakula cha maiti ambacho kinapelekea kusamehewa makosa yake na kupata wepesi katika maisha ya akhera hivyo ni vyema kwa waislamu kuendelea kufanya mambo mema ili kupata radhi za Allah (SW).

 

"Dua  ndio chanzo cha kupata msamaha kwa Mola wetu na kufanyiwa wepesi huko tunakokwenda”alifafanua Waziri Othman.

 

Aidha amefahamisha kuwa Serikali imekuwa ikiendeleza utaratibu wa kuwaombea dua wale wote waliotangulia ambao wameikomboa nchi yetu kwa lengo kuwaenzi viongozi hao .

 

Waziri Shaaban amewaomba wananchi kuwatakia dua waasisi wote waliotangulia kwani wamefanya mengi mazuri kwa ajili ya nchi yao.

 

Hata hivyo Waziri huyo amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Hussein Mwinyi kwa  utaratibu huo wa kuzuru makaburi ya Viongozi waasisi na kuwaombea dua.

 

Akitoa neno la Shukurani mtoto wa Marehemu huyo Daruweshi Khamis Daruweshi ameiomba Serikali kuendelea kuwapatia misaada wazee waasisi ambao bado wapo hai kwa kuthamini kazi kubwa ya kuikomboa nchi. 

 

Marehemu Khamis Daruwesh amezaliwa mwaka 1922 na kufariki tarehe 8 Febuary 2006 na kuzikwa Kijijini kwao KiembeSamaki Wilaya ya Magharibi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.