Habari za Punde

Mashindano ya kuhifadhi Qur-an Jimbo la Shaurimoyo.

Na Takdir Ali. Maelezo Zanzibar.

Wazazi na Walezi nchini wamesisitizwa kuwasimamia watoto kukisoma kitabu kitukufu cha qur-n na kuzingatia mafundisho yake ili kupata fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu.

 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Royal Group Company Hassan Mohammed Raza wakati alipokuwa akitoa nasaha mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kuhifadhi Qur-an Jimbo la Shaurimoyo Wilaya ya Mjini.

 

Amesema qur-an ni chanzo cha kuishi maisha mema na yenye misingi ya imani ambayo ameisisitiza Mtume Muhammad (s a w) hivyo iwapo watakisoma kitabu hicho kitawajengea watoto hao kukuwa katika maadili mem na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

 

Aidha amewasisitiza Walimu na Wanafunzi kuendeleza juhudi walizozianzisha katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kusoma sana qur-an, kutoa zaka na sadala na kusimama katika kisimamo cha usiku.

 

Kwa upande wake Sheikh Abdul-azizi Abdullah Salim el-shuwehdy Imam khatib councilor of muslims affeir of Canada ameeleza kuwa kuisoma qur-an ni kutekeleza moja kati ya nguzo tano za uislam ambapo itawaongoza watoto kuwa waadilifu na kuwajengea hofu ya kumcha Mwenyezi Mungu.

 

Aidha amewataka walimu kujenga tabia ya kuwapa elimu ya dini ya kiislamu na misingi madhubuti ya dini ya Kiislam ili kuendelea kukuza vipaji Vijana wanaohifadhi qur-an tukufu.

 

Mbunge wa Jimbo la Shaurimoyo Ali juma Mohammed amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuwashawishi watoto kuisoma qur-an na kuihifadhi ili kuwawezesha kuwa katika misingi ya imani na dini ya Kiislam.

 

Amesema hali hiyo itaweza kuwajenga Vijana wetu kuwa viongozi wema wa hapo badae na kuwataka wazazi kuongeza juhudi katika kuwasimamia watoto kukisoma kitabu kitukufu cha qur-an.

 

Na Waazi wa Watoto walioshiriki katika Mashindano hayo wamesema wanashukuru uongozi wa Jimbo hilo kwa kusimamia mashindano hayo na kuahidi kuwa wataendelea kukumbusha na kukaa katika vikao vya kheri ili kuisoma qur-an.

 

Mashindano ya kuhifadhi qur-an katika Jimbo la Shaurimoyo yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Ali Juma Mohammed Raza na washiriki wameshiriki kwa uapande wa kuanzia juzuu moja, mbili, tatu, tano, juzuu moja tashjee tahqiiq, tatu tashjee tahqiiq, ishirini na juzuu thelathini ambapo washindi walikabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha Taslim.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.