RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa
mindombinu ya elimu nchini unalengo la kuberesa sekta ya elimu iliyoko kwenye
mageuzi makubwa ya maendeleo.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua skuli ya Sekondari Hassan
Khamis Hafidhi iliopo Mtopepo, Shehiya ya Munduli Wilaya ya Magharibi A, Mkoa
wa mjini Mgharibi, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya miaka
60 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi amesema, nia ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ni kupunguza msongamano wa wanafunzi wengi madarasani na kubakisha
wastani wa wanafunzi 45 kwa kila darasa moja, sambamba na kuweka mkondo mmoja
kwa skuli zote za Unguja na Pemba.
Dk. Mwinyi pia alisema hali hiyo itasaidia matokeo
mazuri kwa kuwepo mazingira mazuri ya kujifunzia.
Akizungumzia mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana
kwenye sekta ya elimu, Rais Dk. Mwinyi ameeleza Sekta hiyo imevuka malengo ya
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2021/ 2025 kwa kuboresha miundombinu ya kisasa,
zikiwemo Makataba, madarasa yenye ubora wa hali ya juu, maabara madawati, kuboeshwa
kwa maslahi ya walimu sambamba na kuongeza ajira za walimu wa hesababati na
sayansi, Unguja na Pemba.
Aidha, Rais Dk. Mwiniyi aliushukuru uongozi wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kufanikisha vyema miradi yote za
Serikali inayosimamiwa na Wizara hiyo kwa kuifanikisha kwa mafanikio makubwa.
Alisema, mradi wa Skuli ya Hassan Khamis Hafidh
licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wake hatimae, umefanikishwa
kwa mafanikio makubwa nakuongeza kuwa ni mradi pekee uliotekelezwa kwa fedha za
uviko 19 kukawia kuzinduliwa hatimae umekamilika ukiwana mafaniko makubwa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa skuli hiyo, Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, ameiahidi Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, kuisimamia kwa ufanisi wa hali ya juu miradi yote inayotekelewa na
kusimamiwa na Wizara hiyo.
Pia, Waziri Lela, amemshukuru Rais Dk. Mwinyi na Dk.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa weledi wao wa
kuendelea kuusimamia na kuudumisha Muungano wa Tanzania ambao kwasasa unatimiza
miaka 60 tokea kuasisiswa kwake mwaka 1964.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar, Khamis Abdalla alisema ujenzi wa Skuli
ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh wa ghorofa tatu ulinza mwezi Februari
mwaka 2022 hadi uliposuasua mwezi wanane mwaka huo na baadae kukabidhiwa Chuo cha
mafunzo kwaajili ya kuuendeleza hadi kukamilika kwake.
Aidha, Katibu huyo amesema ujenzi wa
skuli hiyo umejumuisha madarasa 41, ofisi nne za walimu, ofisi ya mwalimu mkuu,
vyoo 52, maktaba, maabara, chumba cha kompyuta na stoo, na ukumbi mkubwa wa
mikutano.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Chama Cha
Mapinduzi, CCM, Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Magharibi kichama, Muhamed
Rajab Sudi alisifia uongozi wa Rais Dk. Mwinyi na kuuelezea sio uongozi wa
kujionesha bali ni wakuwatumikia wananchi kwa vitendo kama ambavyo mageuzi
makubwa ya maendeleo yanavyoonekana nchi nzima chini ya kipindi kifupi cha
uongozi wake.
IDARA YA MAWASILINO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment