Habari za Punde

mapokezi ya naibu katibu mkuu uvccm mkoa wa kaskazini

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi, akiungana na viongozi wa Vijana na Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika matembezi maalumu yalioanzia Kifumbi kai hadi Ofisi za Chama Mkoa wa Huo Bopwe.
NAIBU Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa ajili ya kuzungumza na Vijana wa UVCCM Mkoa huo.
NAIBU Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mbarwa, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Chama Mkoa huo, kwa ajili ya kuzungumza na vijana wa Mkoa huo.
NAIBU Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi,akipokea taarifa ya umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba kutoka kwa kaimu katibu wa UVCCM mkoa wa Kakazini Pemba Shakila Mwihaji Faki, mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Mkoa huo
NAIBU Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi, akizungumza wakati alipotembelea mradi wa maduka wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Wete
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.