Habari za Punde

Msishangae na Taa za Barabarani za Kijani na Mchoro wa Mtu Inakuruhusu Kuvuka

Msaidizi wa Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Momba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba akiwa na Koplo Baraka Kabala wametoa elimu ya umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Chapwa iliyopo Tunduma Wilayani Momba.

Elimu hiyo imetolewa Mei 09, 2024 ambapo wamewafundisha matumizi sahihi ya kuvuka barabara katika vivuko vya watembea kwa miguu ili waepukane na madhara yanayoweza kuepukika.

Vilevile wamefundishwa kutambua maana ya rangi za taa za barabarani ambapo ikiwa imeoneshwa rangi ya kijani na alama ya mtu mnatakiwa mvuke na hapo mtakuwa salama.

Sambamba na hayo wanafunzi hao wametakiwa kutekeleza kwa vitendo kwa kile kilichowapeleka shule ikiwemo kuepukana na utoro kutokujihusisha na michezo ya kubahatisha (kamali) na madawa ya kulevya ili waweze kufanikiwa katika masomo na malengo yao ya baadae.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.