Habari za Punde

Changamoto za Upatikanaji wa Huduma za Afya Hospitali Binafsi Zajadiliwa

Kaimu Mkurugenzi Idara ya usajili na usimamizi wa Wanachama Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Ali Idrissa Abeid wakati alipokuwa akifungua mkutano wa kujadili Changamoto za utoaji wa huduma kwa watoa huduma wa Hospitali binafsi huko katika Ukumbi wa ZSSF Karaikoo Wilaya ya Mjini.

Na Takdir Ali. Maelezo. 03-06-2024.

Watoa huduma wa Hospitali binafsi Zanzibara wametakiwa kufuata utaratibu na Sheria ziliowekwa na Serikali kupitia Mfuko wa huduma za afya Zanzibar (ZHSF) ili kuepuka vitendo vya Udanganyifu.

 

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya usajili na Usimamizi wa Wanachama Ali Idrisa Abeid wakati alipokuwa akifunguwa kikao cha kujadili Changamoto za utoaji wa huduma katika Hospitali binafsi huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Wilaya ya Mjini.

 

Amesema kuna baadhi ya Watoa huduma, wanafanya kinyume na maelekezo waliopewa na ZHSF jambo ambalo linasabisha kuwepo kwa viashiria vya udanganyifu.


Aidha amewaomba Watoa huduma hao, kuwacha kuwandikizia wagonjwa dawa zisiohusiana na maradhi yao kwani kufanya hivyo ni kiwatengenezea usugu wa dawa sambamba na kuwasababishia maradhi mengine ikiwemo kufeli kwa figo.

 

Kwa upande wake Afisa udhibiti ubora wa huduma kutoka Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Dkt. Daud Suleiman Daud amewataka Madaktari hao kutoa elimu kwa Wagonjwa wao kabla ya kuwapa matibabu ili kuepuka migongano baina yao.

 

“Wagonjwa wetu hatuwapi elimu yoyote na wanakuwa hawajuwi maradhi yanayowasmbu, vipimo wanavyofanyiwa na wakati mwengine wanashindwa hata kujielezea.” Alisema Dkt. Huyo.

 

Hata hivyo amesema endapo Madaktari hao watabadilika na kuwa wawazi kwa Wagonjwa wao, itawasaidia wagonjwa kuelezea changamoto walizonazo na kuepukana na malumbano na Watoa huduma hao.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Watumiaji wa Mfuko wa ZHSF wameomba kuwekewa kipindi cha kufanya uchunguzi kwa Wanachama wao ili kuweza kutambua matatizo mapema yanayowasumbua na sio kusumbiri maradhi kuwa makubwa.

 

Wakichangia mada katika kikao hicho baadhi ya Watoa huduma wa Hospitali binafsi wamelalamikia baadhi ya Wazee kuwaachia Watoto kuenda hospitali pekeyao jambo ambalo linawapa usumbufu hasa wakati wa kutoa maelezo na kutia Saini.

Afisa Madai kutoka Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Sabra Mohammed akichangia katika Mkutano wa kujadili changamoto za utoaji wa huduma  kupitia hospitali binafsi huko Ukumbi wa Zssf Karaikoo Wilaya ya Mjini.
Afisa udhibiti ubora wa huduma kutoka  Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Dkt. Daud Suleiman Daud akiwasilisha mada ya viashiria vya udanganyifu wakati wa utoaji wa huduma katika mkutano uliowashirikisha watoa huduma wa hospital binafsi huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Wilaya ya Mjini.
Mshiriki kutoka hospital ya Afya first Ndg. Nassor Said Wazir akichangia katika mkutano wa kujadili changamoto za utoaji wa huduma kupitia hospitali binafsi huko katika Ukumbi wa Zssf Karaikoo Mjini Zanzibar.
Mshiriki kutoka hospital ya TASAKHTA  Wastara Ahmed akichangia katika Mkutano wa kujadili changamoto za utoaji wa huduma  kupitia hospitali binafsi huko Ukumbi wa Zssf Karaikoo Mjini Zanzibar.
Mshiriki kutoka hospital ya Raudhwa Samira Khamis Mohammed akichangia katika mkutano wa kujadili changamoto za utoaji wa huduma  kupitia hospitali binafsi huko katika Ukumbi wa Zssf Karaikoo Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.