Habari za Punde

Ujumbe Kutoka Zanzibar Wapata Mafunzo Kuhusu PPP

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiongoza kikao kazi kilichojadili kuhusu Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, masuala mbalimbali kuhusu Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi na utekelezaji wa Sera ya Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), wakati wa kikao kazi na ujumbe wa Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Rashid Ally Salim (kushoto), katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Kitengo cha PPP, Bw. Bashiru Taratibu.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, amekutana na ujumbe wa Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Rashid Ally Salim, katika kikao kazi kilichojadili kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) majukumu ya Kitengo cha PPP, masuala mbalimbali kuhusu Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Rashid Ally Salim, akieleza madhumuni ya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wizara ya Fedha kuwa ni pamoja na kujifunza kuhusu utekelezaji wa Sera ya Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) na Majukumu ya Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Ofisini kwake, jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bi. Fadhila Hassan Abdalla.
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, akieleza majukumu ya Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ambayo ni pamoja na kusimamia Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), wakati wa kikao kazi na ujumbe wa Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Rashid Ally Salim, jijini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu (wa nne kushoto), akitoa maelezo ya utendaji kazi kati ya Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi wakati wa kikao kazi na ujumbe wa Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Rashid Ally Salim (wa pili kulia), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Rashid Ally Salim (wa pili kushoto), wakiwa na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji baada ya kikao kazi kuhusu utekelezaji wa Sera ya Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Rashid Ally Salim (katikati), akiwa na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji baada ya kikao kazi kuhusu utekelezaji wa Sera ya Sera ya Taifa ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.