Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amekutana na Uongozi wa ZRCP Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Utafiti cha Mambo ya Jamii,Uchumi na Sera, ukingozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Ndg,Juma Hassan Reli (kushoto kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 17-7-2024. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti cha Mambo ya Jamii,Uchumi na Sera. Ndg.Juma Hassan Reli (kushoto kwa Rais) akiwa na ujumbe wake mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 17-7-2024 na (kulia kwa Rais) Bi. Rukiya Wadoud.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema lazima yafanyike mabadiliko katika uendeshaji wa Serikali ili kuendana na mageuzi ya uchumi wa kidijitali

Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 17 Julai 2024, alipokutana na  Uongozi wa Kituo cha utafiti wa sera na uchambuzi Zanzibar (ZRCP) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Juma Hassan Reli Ikulu Zanzibar. 

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewataka  ZRCP kutafuta njia mbadala wa kusimamia utekelezaji wa tafiti zinazofanyika katika sekta mbalimbali.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amekubali ombi la ZRCP kushiriki kufungua Mkutano wao mkuu wa mwaka utaofanyika tarehe 5 Septemba 2024.

Naye  Juma Hassan Reli ameeleza kuwa  miradi ya maendeleo imetekelezwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dkt.Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.