Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleima Abdulla akizungumza na viongozi na watendaji kutoka Taasisi za Ufuatiliaji na Tathmini kutoka katika serikali ya SMT na SMZ kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika ufunguzi wa Kongamano la Tatu(3) la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza liliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Jijini Zanzibar.
Serikali ya SMT na SMZ zitaendelea na juhudi za kuimarisha dhana ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa pande zote mbili za Muungano hasa katika shughuli za Mipango ya Kitaifa na Miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na na Mkamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua Kongamano la Tatu(3) la Kitaifa la wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi liliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesem Tanzania inaendele kupiga hatua katika uimarishaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini ikiwemo kuweka mifumo na miundombinu yenye kuwezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa Taasisi za Kitaifa zinazoratibu masuala hayo kwa maslahi mapana ya nchi.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed amesema matumizi ya Teknoloji katika kufanya ufuatiliaji na Tathmini kutaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuimarisha uwajibikaji na kuongeza kasi na uwazi katika kuleta ustawi wa wananchi kwa kutoa huduma sahihi za kijamii na kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa anatambua kuwa mafanikio makubwa yamepatika katika shuhuli za ufuatiliaji na tathmini nchini hivyo amezitaka Mamlaka husika kufanya jitihada za kukamilisha maandalizi ya Sera za Ufuatiliaji kwa Serikali zote mbili pamoja na kutenga rasilimali za kutosha kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini.
Aidha amezitaka Taasisi hizo kuhakikisha taarifa zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji na Tathmini zinatumika katika kufanya maamuzi na kuweka mikakati Imara ya kuhabarisha Umma juu ya matokeo ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa kushirikiana na waandishi wa habari ili kufikia malengo ya taasisi na taifa kwa ujumla.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed ametowa wito kwa chama cha Wataalamu Afrika ( AFrEA) kuendelea kuvilea vyama vidogo vidogo vilivyomo nchi wanachama pamoja na kuapta fursa za kujifunza na kujiimarisha ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratib na Bunge Mhe. William Vangimembe Lukuvi amesema katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini kunahitaji uwepo wa taasisi zenye kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ili kusaidia kulinda matumizi ya rasilimali fedha zinazotumika katika miradi hio.
Mhe. Lukuvi amesema kuwepo kwa Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza vinaakithi dhamira ya Serikali zote mbili ya kuhakikisha mabadiliko na marekebisho makubwa yanafanyika katika kuimarisha Teknolojia na mifumo ambayo itasaidia kufikia malengo yaliyowekwa na serikali hizo kwa maslahi mapana ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.
Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amesema kufanyika kwa Kongamano la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza hapa Zanzibar litaibua na kupendekeza njia nzuri zaidi za kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini hasa katika masuala ya Utalii na Uwekezaji nchini.
Mhe. Sharif amesema kufanyika kwa Ufuatiliaji na Tathmini kunasaidia katika kupima shuhuli za mipango ya maendeleo ya Kimataifa, kitaifa na Kikanda kwa kutathmini ufanisi na uwajibikaji wa Taasisi husika hasa katika kupata taarifa na Takwimu sahihi zenye matokeo chanya ya mipango hio.
Imetolewa na Kitengo Cha Habari ( OMPR)
Leo Tarehe 17. 09. 2024.
No comments:
Post a Comment