Habari za Punde

Baraza la Taifa la Biashara limesaidia kuweka Mazingira mazuri ya kibiashara - Dk Mwinyi

Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Jukwaa la Kumi na Tatu(13 )la Biashara  lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege,Kiembe samaki Zanzibar.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shabani akitoa maelezo katika hafla ya Jukwaa la Kumi na Tatu(13) la Biashara lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege,Kiembe samaki Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Jukwaa la Kumi na Tatu(13) la Biashara  lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege,Kiembe samaki Zanzibar.
 


PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.12/10.2024.

Na Khadija Khamis – Maelezo .12/10/2024.

 

Mwenyekiti wa  Jukwaa la Biashara Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema  kuanzishwa kwa Baraza ya Taifa la Biashara  kumesaidia kuweka  Mazingira mazuri ya kibiashara nchini.  

 

Amesema hayo katika Mkutano wa Jukwaa la kumi na tatu la biashara katika ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar .

 

Amesema Serikali imeanzisha Jukwaa la Biashara kwa kuweka mfumo wa majadiliano na mashirikiana kwa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuweka mazingira mazuri ya wafanya biashara .

 

Amefahamisha kuwa lengo la jukwaa hilo ni kupanua wigo wa wafanyabiashara pamoja na kuondosha changamoto zinazojitokeza .

 

Vilevile ameeleza kuwa serikali imeimarisha huduma za   utoaji wa risiti za electroniki kwa sekta za umma  sambamba na kuondoa kodi za thamani kwa wafanyabiashara wanaoingiza biashara zao.

 

Amesema Serikali imeweza kusimamia  ulipaji wa viwango vipya vya mshahara kwa sekta binafsi pamoja na utaratibu wa kulipa kima cha chini cha Mshahara kwa Wafanyakazi pamoja na kuimarisha huduma za bandari.

 

Nae Waziri wa Biashara  na Maendeleo ya Viwanja .Mhe Omar Said Shaaban amewataka wafanyabiashara kutumia fursa za majadiliano ikiamini kwamba serikali itasikiliza changamoto zinazopo na kuzifanyia utekelezaji .

 

Ameeleza kuwa Wizara ya Biashara itaendelea kuwapatia mazingira wezeshi wafanya biashara hao ili kuepukana na changamoto .

 

Nao washiriki wa Jukwaa hilo walielezea changamoto mbali mbali zinazochangia  kuzorotesha  Biashara zao ikiwemo  ucheleweshaji wa utoaji wa makontena pamoja mfumo ambao sio rafiki wa ulipaji kodi wa bidhaa zao

 

Kauli mbinu ya Jukwaa la kumi na tatu ni Kuimarisha Sekta Binafsi katika Uchumi wa Buluu.”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.