Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Awasili Nchini Hispania kwa Ziara ya Kikazi



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Othman Masoud Othman  amewasili Nchini Hispania akitokea Zanzibar - Tanzania.

Akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Madrid, Mhe.Othman ambaye ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, wamepokelewa na Maafisa wa Kibalozi wakiongozwa na  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Bw. Ally Jabir Mwadin.

Mhe.Othman yupo Nchini Spain kwa Ziara Maalum ya Kikazi, ambapo pia atashiriki Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Utalii wa Bahari, Mazingira na Uchumi wa Buluu, huko Mjini Almeria.

Katika Ziara hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana pia na Viongozi mbali mbali wa Serikali, akiwemo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Soraga na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendeshaji na Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA), Ndugu Sheha Mjaja Juma.

Kitengo cha Habari 

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Novemba 18, 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.