Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAZISHI YA MZEE JOHN TUTUBA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba alipowasili Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kushiriki mazishi. Tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Novemba 2024 ameshiriki mazishi ya marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba yaliyofanyika kijijini kwake Kibondo mkoani Kigoma. Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Wilayani Kibondo na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhashamu Askofu Joseph Mlola.

Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Rais amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Makamu wa Rais amesema marehemu mzee John Tutuba alikuwa mtumishi mwaminifu wa umma katika nafasi zote alizowahi kuzitumikia enzi za uhai wake. Amesema pia aliwatunza vyema watoto wake katika maadili na kuhakikisha wanapata elimu na hivyo kutumika kulisaidia Taifa.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi kujenga tabia ya kuhakikisha watoto wao wanapata elimu itakayowasaidia wao na Taifa kwa ujumla. Aidha amewasihi watanzania kutimiza wajibu wao katika jamii ikiwemo kuwaenzi na kuwatunza wazazi na walezi wao pindi wanapohitaji msaada.

Makamu wa Rais ametoa wito wa kuwajenga watoto katika maadili mema yatakayoanzia katika imani za dini.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

06 Novemba 2024Kibondo, Kigoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Gavana wa Benki Kuu (BOT) Emmanuel Tutuba wakati wa mazishi ya baba yake mzazi marehemu John Tutuba yaliyofanyika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi kwa waombolezaji mbalimbali marqa baada ya Ibada ya kumuaga marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya kumuaga marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi kwa waombolezaji mbalimbali marqa baada ya Ibada ya kumuaga marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba wakati wa Mazishi yaliyofanyika Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka mchanga katika kaburi la John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (B0T) Emmanuel Tutuba wakati wa Mazishi yaliyofanyika Kibondo mkoani Kigoma tarehe 06 Novemba 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.