Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Masoud Ali Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara hio kutimia miaka Minne (4)ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Na Takdir Ali. Maelezo. 06.11.2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Massoud Ali Muhammed amewataka Wananchi wasikubali kutapeliwa kwa madai ya kupatiwa ajira za Vikosi.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Karume house, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, ikiwa ni kuelezea mafanikio yaliopatika kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Amesema ajira za Serikali haziuzwi na zimewekwa Mfumo nzuri wa kuajiri hivyo amewatahadharisha Wanachi kutokubali kutapeliwa kwa madai ya kupatiwa ajira.
Hata hivyo amesema Serikali haitomfumbia macho mtu yoyote atakaebainika kufanya utapeli na kuwaomba Wananchi kuwaripoti watakaowabaini kufanya vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Aidha amesema jumla miradi 64 imetekelezwa kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Hata hivyo amesema licha Idara maalum kutekeleza jukumu la msingi la kulinda Amani na Utulivu lakini pia imeweza kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Masoko, Elimu na Uchumi wa Buluu.
Mbali na hayo amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya Barabara, Serikali inakusudia kuanzisha mradi maalum wa usafi, utakaotumia vitendea kazi vya kisasa.
Amebainisha kuwa Serikali imetumia fedha nyinyi kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko hivyo haitomfumbia macho mtu ataefanyabiashara katika maeneo yasioruhusiwa ikiwemo Barabarani.
Mbali na hayo Mhe. Massoud amewaomba Waandishi wa Habari kuisaidia Serikali katika kuelimisha jamii juu ya suala hilo.
No comments:
Post a Comment