Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan akiongoza Mkutano wa Dharura wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
tarehe 28 Januari, 2025.
Katika Mkutano huo, Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki pamoja na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema sambamba na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera. Aidha, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi walishiriki kwa njia ya mtandao.
No comments:
Post a Comment