Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amefungua Skuli ya Msingi ya Ghorofa Abeid Amani Karume Mwera

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa (kushoto) kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika 12-3-2025, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karumeu Mwera Wilaya ya Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika  12-3-2025 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Muhammed Mussa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwanafunzi Adam Simai Uwesu wa Darasa la Sita Skuli ya Msingi Mwera,  akitowa maelezo ya matumizi ya vifaa vya Maabara wakati akitembelea maabara ya Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume 12-3-2025, baada ya kuifungua 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma vitabu wakati akiwa katika chumba cha Maktaba ya Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kuifungua 12-3-2025.akiwa na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mwera wajisomea vitabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma vitabu wakati akiwa katika chumba cha Maktaba ya Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kuifungua leo 12-3-2025.akiwa na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mwera wajisomea vitabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi na Wanafunzi, baada ya kuifungua Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika 12-3-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika 12-3-2025.
WANANCHI na Walimu mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja ufunguzi huo uliyofanyika  12-3-2025.
WANANCHI na Walimu mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja ufunguzi huo uliyofanyika  12-3-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika 12-3-2025.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali vu Mwinyi amesema Serikali   itaendelea Kuimarisha Miundonbinu ya Sekta ya Elimu kwani ndio Kipaumbele cha kwanza cha  Serikali anayoiongoza.

Rais Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo  wakati wa Ufunguzi wa Skuli Tatu Mpya za Msingi za Ghorofa za Chumbuni, Kidichi na Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume  iliopo Mwera.

Rais Dkt, Mwinyi  amefahamisha kuwa Serikali inajikita  Kuimarisha Sekta ya Elimu kuanzia ngazi ya Msingi , Sekondari na Vyuo Viikuu  kwani ni nyenzo Muhimu ya kufanikisha Maendeleo katika Sekta zote.

Amebainisha kuwa kwa Muda mrefu Zanzibar ilikuwa ikikabiliana na Changamoto  Tatu kuu katika Sekta ya Elimu ambazo Serikali imeamua kuziondosha.

Amezitaja Changamoto hizo kuwa  ni Ukosefu wa Miundonbinu ya Elimu iliobora, Upungufu wa  Walimu hususani wa Masomo ya Sayansi pamoja na Ukosefu wa Vifaa vya  kufundishia na Kujifunza ambazo kwa Kiwango kikubwa  zilidhorotesha  Maendeleo ya Elimu hapa Nchini.

Dkt, Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali itaendelea na Ujenzi wa Skuli za ghorofa katika maeneo mbalimbali  pamoja na Kuongeza Idadi ya Walimu sambamba na Kuimarisha Maslahi Yao  ili watekeleze Majukumu Yao kwa Ufanisi zaidi.

Aidha  amefahamisha kuwa Serikali inakusudia kuzifanya Skuli zote kuwa na Viwango Bora vya kujifunzia kwa kuwa na Vifaa vya kutosha vya kujifunzia, Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta Ili kuwaandaa Wanafunzi katika ngazi za awali.

Rais Dkt, Mwinyi ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa Usimamizi Bora wa Ujenzi wa Skuli hizo Tatu pamoja  na Uongozi wa Wilaya na Mikoa kwa Ufuatiliaji wa  Miradi Hiyo.

Rais Dkt, Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa kamwe  hatayumbishwa  na Kauli potofu za  Watu  Wasiopenda Maendeleo katika dhamira yake ya Kuleta Maendeleo na Mabadiliko  katika Sekta ya Elimu.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa  amesema Mageuzi Makubwa yanayoendelea katika Sekta ya Elimu  yanasaidia  Kuongeza Ufanisi katika Utekelezaji wa Mtaala Mpya wa Elimu na Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi.

Akiwasilisha Taarifa ya Kitaaluma ya Ujenzi wa Skuli hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla amesema kila Skuli imegharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5 hadi kukamilika zikiwa na Madarasa 29 kila Moja , Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.