Habari za Punde

Wafanyakazi Watakiwa Kutunza Nidhamu Uweledi na Uwadilifu ili Kuimarisha Ufanisi wa Kazi Zao

Mfanyakazi wa Wizara ya  Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo , Bakari Khamis Mkanga akiuliza suali kwa Muwasilishaji Yahya Saleh Salim kutoka Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria,Utumishi na utawala bora  (wa pili kulia  ) huko Migombani, Wilaya ya Mjini.

Muwasilishaji mafunzo Yahya Saleh Salim kutoka Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora akitoa elimu kwa wafanyakazi wa Wizara ya  Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo , huko Migombani, Wilaya ya Mjini.
Afisa Maslahi kutoka Ofisi ya Rais ,Katiba ,Sheria,Utumishi na Utawala Bora,Mustafa Khamis Simai akiwafahamisha upimaji na tathimini watumishi wa  Wizara ya  Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo , huko Migombani, Wilaya ya Mjini.

Imetolewa na Kitengo cha Habari

WHVUM.

Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo , Rashid  Makame Hamdu amewataka wafanyakazi  kutunza nidhamu uweledi na uwadilifu ili kuimarisha ufanisi wa kazi zao.

Ameyasema hayo wakati  akifungua mafunzo ya kukumbushana  juu ya Sheria za kazi kwa watumishi wa Wizara hiyo huko Migombani, Wilaya ya Mjini.

Amesema kuwa iwapo wafanyakazi  watafuata sheria za utumishi wa kazi kwa kutunza nidhamu, uweledi, uwadilifu pamoja na uwajibikaji kutasaidia kujiamini katika utekelezaji wa Majukumu yao  .

‘’Kila mtumishi anapaswa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili tuweze kufIkia malengo ya kiutendaji   ’’ amesema Mkurugenzi Rashid.

Nae Muwasilishaji mada kutoka Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Yahya Saleh Salim amesema asiyetii sheria pamoja na miongozo ya kiutumishi atakuwa amevunja maadili na miko.

Aidha amewafahamisha watumishi hao kutotoa taarifa za serikali au siri za serikali kwa watu wasiohusika jambo mbalo ni kosa la kimaadili .

Alieleza kuwa ni kosa kutoa  taarifa za ndani, matumzi mabaya ya Ofisi pamoja na kufanya udhalilishaji dhidi ya muajiri mwengine.

Aliwataka wafanyakazi hao kudumisha maadili mema na kufuata masharti yaliyowekwa katika kanuni ikiwemo kufanyakazi kwa kuzingatia wakati na ufanisi .

Nae Afisa Maslahi kutoka Ofisi ya Rais ,Katiba ,Sheria,Utumishi na Utawala Bora,Mustafa Khamis Simai amesema ni wajibu wa kila mtumishi wa umma kufanyiwa upimaji na tathmini katika utekelezaji wa kazi zake za kila siku ili kupatikana  haki zake .

Aidha amesema Serikali haitofanikiwa bila ya wafanyakazi kutekeleza majukumu yao kiufanisi na kujiepusha na uzembe ambao utasababisha kuishushia hadhi Afisi na Mtumishi wake  .

Akiwaasa watumishi hao kutofanya  vitendo ambavyo vitapelekea kujivunjia heshima sambamba na kujiingiza kwenye madeni ambayo Mtumishi atakayoshindwa  kuyalipa .

Akielezea kanuni ya 33(1)-(3)inayozungumzia kutotumia vileo na kuwaonya watumishi kujiepusha na matumizi ya vileo, uvutaji wa sigara matumizi ya madawa ya kulevya, uraibu na aina yoyote ya vileo katika sehemu za kazi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.