Habari za Punde

Uongozi Zanzibar SUKUK kupitia PBZ kufanya jitihada zaidi za kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma za SUKUK

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameutaka uongozi Zanzibar SUKUK kupitia PBZ kufanya jitihada zaidi za kutoa elimu kwa umma  kuhusu huduma za SUKUK kupitia Benki hiyo ili kusaidia kuukabili ushindani mkubwa uliopo katika biashara ya fedha hapa nchini.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake migombani mjini Zanzibar alipokutana na ujumbe wa PBZ uliofika kwa mazungunzo kuhusiana na mradi wa uwekezaji wa SUKUK kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ IKHILAS.

Amefahamisha ili kupata ufanisi kupitia huduma za BPZ IKHILAS kunahitajika kujengwa uelewa mkubwa kwa jamii hivi sasa katika kuendesha na kusimamia biashara za fedha na uwekezaji wa aina hiyo  sambamba na kujitahidi kujenga uwezo kwa watendaji mbali mbali  walionao katika kukabili biashara kwa mbinu za kisasa zaidi.

Amesema kwamba kuna haja kubwa benki ya PBZ  kuyatumia majukwaa ya kidijitali kujitahidi kuwafikia wananchi waliowengi zaidi ambao ndio wateja na wateja watarajiwa wa huduma za benki hiyo kwa uwekezaji miradi kama ya SUKUK ikiwemo huduma za mikopo na nyenginezo zinayoanzishwa  ndani ya benki hiyo kupitia PBZ Ikhilas inayozingatia misingi ya uislamu.

Amesema katika kipindi hiki chenye ushindani mkubwa wa kibiasara za fedha ni vyema watendaji na viongozi wa Benk hiyo kuwa wabunifu zaidi na kutumia maarifa na elimu kuchangia maendeleo makubwa ya Benki hiyo ambayo ni miongoni mwa benki kongwe nchini Tanzania.

Amesema kwamba Zanzibar zipo fedha nyingi kutoka mikononi mwa wananchi  zinazoweza kuwekezwa lakini azijafanyiwa ivyo kutokana na sababu zao mbali mbali za kidini walizonazo wananchi na kwamba elimu ni jambo pekee linaloweza kubadili mazingira  na mwelekeo wa namna hiyo kwa jamii. 

Hata hivyo, Mhe. Makamu amesema kwamba huduma za PBZ IKHILAS zinaitajika sana ndani ya jamii ya Zanzibar katika kubadili mfumo wa kiuchumi wa wanajamii uliozoeleka hapa Zanzibar  iwapo watakuwa na elimu ya kutosha.

Aidha amewataka ujumbe huo kujaribu kuainisha uwezo na changamoto na matatizo mbali mbali waliyonayo  yanayohitaji ufumbuzi wa serikali kuu kuyawasilisha pamoja na mapndekezo yake ili yatatauliwe.

Naye Mkurugenzi wa PBZ Ikhlas Rajab Mohammed Ramia aliyeongoza ujumbe huo, amesema kwamba Mradi wa Zanzibar SUKUK unalengo la kukuza uwekezaji katika biashara   ya fedha na huduma za kijamii kwa misingi ya uislamu.

Amesema kwamba huduma za uwekezaji wa skuk imeazna kutolewa hapa Zanzibar kupitia PBZ IKHILAS kwa   takribani miaka mitano iliyopita kwa taasisi za watu binafsi ambazo zimefanikiwa sana katika mwelekeo wa kukuza Mipango ya Benki ya kiislamu. 

Amesema kwamba

Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar kupitia Kitengo cha habari leo jumanne Machi 26, 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.