Habari za Punde

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- UFUNGUZI USHIRIKISHO WA MKUTANO WA SHIRIKISHO LA KIATAIFA

Na.OMPR.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zitaendelea kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mawakala wa Ushuru na Forodha kwa Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati.

Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi Mkutano wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mawakala wa Ushuru na Forodha kwa Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati wa mwaka 2025, uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip.

Amesema Shirikisho la Vyama vya Mawakala wa Ushuru na Forodha, limekuwa likifanya kazi kubwa ikiwemo kuandaa mikutano na kusaidia vyama vya Mawakala wa Ushuru na Forodha Duniani katika kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa Mikataba, Sera na Sheria za Kimataifa.  

Mhe. Hemed amesema ushirikiano uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wadau wa Sekta ya Uchukuzi umewezesha ongezeko la mzigo inayopitia chini kuelekea nchi jirani.

Amesema kutokana na hali hiyo, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbali mbali ikiwemo kuboresha mifumo, kujenga na kukarabati miundombinu, kushirikisha Sekta binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari na kutoa elimu binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari.

Amefahamisha kuwa muda wa kuhudumia meli za makasha katika bandari umepungua kutoka wastani wa siku 10, hadi siku tatu na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za bandari na Kodi ya forodha kutoka shilingi trilioni 7.08 2024 kufikia shilingi trilioni 8.26 kwa mwezi Februari mwaka 2025.

Amesema Serikali ya Awamu ya sita inaendelea na utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo ni wezeshi katika sekta ya Uchukuzi inayojumuisha ujenzi wa reli ya kisasa, ukarabati wa viwanja vya ndege na vivuko kwa lengo la kuunganisha huduma na miundombinu ya Uchukuzi.

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imefanya maboresho makubwa kwenye sekta ya Uchukuzi na kuweza kupata mafanikio chanya ambayo yameleta mabadiliko makubwa katika utoaji wahuduma.

Makamu huyo amesema miundombinu ya Uchukuzi ikiwemo kuongezeka kwa meli za kigeni na utoaji wa mzigo, ujenzi wa bandari ya Shumba Mjini, Bandari ya Kizimkazi, Bandari jumuishi ya Mangapwani, Bandari ya Wete na Bandari ya abiria ya Mpigaduri.

Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha Sekta ya Uchukuzi inaimarika katika utoaji wa huduma inaendelea na ujenzi wa miradi ya Miundo ya usafiri ili kuunganisha huduma za usafiri na usafirishaji ikiwemo ujenzi wa kiwanja kipaya cha ndege Kisiwani Pemba.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt. Khalid Salum Mohammed, amesema Serikali imedhamiria kukuza sekta ya Usafirishaji, Lojistiki na Uchumi wa Buluu kwa kuimarisha miundombinu ya Bandari, kuimaisha huduma za ushuru wa forodha na kuimarisha mazingira ya kibiashara.

Dkt. Khalid amefahamisha kuwa Serikali inatekeleza miradi ya kimkakati kupitia uwekezaji wa miundombinu ya Bandari yenye kuzingatia utunzaji wa mazingira na uwekaji wa matumizi ya mifumo ya utoaji wa huduma za bandari zenye ufanisi na za kidijitali, ambazo hurahisisha utoaji wa huduma na kudhibiti mapato.

Amesema lengo la Serikali ni kukuza ushirikiano na nchi mbali mbali na sekta binafsi, katika kuimarisha sekta ya uchukuzi na lojistiki kwa kuzingatia viwango ya kimataifa.

Naye Rais wa Chama cha Makala wa Ushuru na Forodha Tanzania, Edward Urio, amesema kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji ikiwemo mageuzi katika Bandari ya Dar es Salaam, uboreshaji wa Bandari kwa kutumia vifaa vya kidijitali ambavyo vinaiwezesha Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika hiyo.

Urio amesema kuna umuhimu wa kuwepo ushirikaano kwa nchi za Afrika hasa katika masuala ya kupeana taaluma, ujuzi na kubadilishana uzoefu kwenye matumizi ya teknolojia katika sekta ya usafirishaji, utalifanya bara hilo kupiga hatua.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 30.04.2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.