RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Sera
ya Biashara 2024 na Tathmini ya Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara (Zanzibar
Blue Print )2025, uzinduzi huo uliyofanyika leo 30-4-2025 katika ukumbi wa Hoteli
ya New Amaan Complex Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameahidi Serikali kuviondoa Vikwazo vyote vinavyochangia Kukwamisha Uendeshaji wa Biashara hapa nchini.
Rais Dkt,Mwinyi amesema hayo alipoizindua Sera ya Biashara ya 2024 na Tathmini ya Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara (Zanzibar Blue Print) 2025 Hafla iliofanyika New Amani Hotel , Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 30 Aprili 2025.
Aidha Rais Dkt, Mwinyi amebainisha kuwa bado lipo Tatizo la kuwepo kwa Urasimu,Ucheleweshaji wa Watu kufanya Biashara zao na Utendaji usio na Ufanisi kwa baadhi ya Watendaji katika Sekta ya Biashara.
Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali haiwezi Kuendelea na Watendaji wanaosababisha kuwepo kwa Vikwazo katika Uendeshaji wa Biashara.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amewatoa hofu Wadau na Taasisi zinazosimamia Sekta ya Biashara kuwa Serikali imedhamiria kuweka Mazingira mazuri ya Ufanyaji wa Biashara.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa Sera ya Biashara na Ripoti ya Tathmini lazima kuwepo na Msimamizi Mwenye dhamira ya Kweli ya kusimamia Utekelezaji wa Sera Hiyo na kuahidi kulivalia njuga Suala Hilo na Utekelezaji wa Sera Hiyo.
Ameziagiza Taasisi zote za Umma na Binafsi kutekeleza kikamilifu Sera ya Biashara 2024 na tathmini ya Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara.(Zanzibar Blue Print) 2025.
Akizungumzia Uzinduzi huo wa Sera amesema itasaidia kwa kiwango kikubwa kuleta Ufanisi wa Utekelezaji wa Sekta ya Biashara na kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha Biashara.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt Mwinyi amesema kuwa Sera hiyo ni hatua ya Kufanikisha Ahadi ya Ilani ya CCM ya 2020-2025 ilioitaka Serikali Kuandaa Mazingira Bora ya Biashara Nchini.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu ya Mlango wa
Zanzibar na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said
Shaban, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Biashara 2024 na Tathmini ya
Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara (Zanzibar Blue Print)2025, uzinduzi huo
uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya New Amaan Complex Zanzibar leo 30-4-2025.

No comments:
Post a Comment