Habari za Punde

RAIS MWINYI:MKUTANO WA MAJAJI(SEACJF) NI FURSA MUHIMU KUIMARISHA UTENDAJI WA MAHAKAMA

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na  ujumbe wa Jopo la Majaji wa Jumuiya ya Ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afrika (SEACJF) ukiongozwa na Jaji Mkuu wa Eswatini Mhe.Moses Cuthbert Maphalala (kulia kwa Rais)  mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-4-2025 na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(SEACJF) unaotarajiwa kufanyika Zanzibar  Mwakani  Ni fursa Muhimu ya Kuimarisha Ushirikiano na Kuimarisha Utendaji wa Mahakama kwa Nchi hizo.

Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Jopo la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika Waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 28 Aprili 2025.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa mbali na kuwaleta pamoja Mkutano huo utasaidia kubadilishana Uzoefu Baina ya Nchi na Nchi na Kujadili kwa pamoja Changamoto za Kiutendaji wa Mahakama kwa Nchi wanachama.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Majaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kutoa Ushirikiano wa kutosha kufanikisha Mkutano huo wa Kwanza kufanyika Nchini.

Amewasisitiza Majaji hao wakati wa Mkutano huo kuvitembelea Vivutio vya Utalii vya Zanzibar na hatimaye kuwa Mabalozi Wazuri wa kuitangaza Zanzibar katika Nchi zao hatua itayochochea Kukuza Sekta ya Utalii inayochangia asilimia 30 ya pato la Taifa.

Naye, Rais wa Jumuiya Hiyo Jaji Mkuu wa Eswatini Moses Cuthbert Maphalala amesema lengo Kuu la Mkutano huo ni Kulinda na Kuimarisha Utawala wa Sheria ,Uhuru wa Mahakama , kubadilishana Uzoefu pamoja na kuhakikisha mihimili ya Nchi inafanya Kazi kwa Pamoja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu ya kitabu,kutoka kwa Jaji Mkuu wa Kenya Mhe.Martha Koome, baada ya kumaliza mazungumzo yake ya wageni wake Jopo la Majaji kutoka Jumuiya ya Ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afrika (SEACJF) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-4-2025.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Jopo la Majaji wa Jumuiya ya Ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afrika (SEACJF) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-4-2025.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.