Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali
bungeni wakati wa Kikao cha 23 Mkutano wa 19 wa Bunge jijini Dodoma leo tarehe 13
Mei, 2025.
Serikali imefanya tathmini ya kina ya hali ya mazingira ya Ziwa Tlawi lililopo mkoani Manyara na kuandaa taarifa iliyobainisha changamoto mbalimbali ambazo zinatishia uhai na uwepo wa ziwa pamoja na mifumo ikolojia yake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis leo tarehe
13 Mei, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu
Mjini Mhe. Zacharia Issaay aliyetaka kujua hatua gani imefikiwa
katika kutekeleza taarifa ya wataalamu kuhusu Ziwa Tlawi.
Mhe. Khamis amesema miongoni mwaa changamoto zilizobainishwa ni ziwa kujaa tabaki (tope), kupungua kwa maji yanayoingia ziwani kunakotokana na uchepushwaji wa maji yote ya Mto Endayaya ambayo yanatumika kwa shughuli za majumbani.
Pia, ametaja uwepo wa magugu maji ya aina mbalimbali ndani na
kandokando ya ziwa ni changamoto zinazosababisha kupunguza eneo la shughuli za
uvuvi pamoja na bayoanuai ikiwepo samaki.
Aidha, Mhe. Khamis amesema katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali itaendelea kutenga
fedha pamoja na kutafuta fedha kupitia mifuko ya hifadhi na usimamizi wa
mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Mfuko wa Dunia wa
Hifadhi ya Mazingira (GEF) na Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
(GCF) ili kunusuru ziwa hilo na mifumo ikolojia yake.
“Kwa
kutambua athari ambazo zinaweza kusababishwa na uharibifu wa Ziwa Tlawi na
maziwa mengine hapa nchini, kupitia Bunge lako tukufu ninaomba kuziagiza halmashauri
zote nchini kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi
wa Mazingira Sura 191 kifungu namba 57 (4) (i) kinachozuia kuendesha shughuli
za kudumu za binadamu au zenye madhara kwa mazingira ndani ya mita sitini
kutoka kwenye kingo za ziwa hilo pamoja na mito na vijito vinavyochangia kujaa
maj,” alisema.
Katika hatua nyingine, akijibu swali la nyiongeza kuhusu
hatua za Serikali za kukabiliana na changamoto hizo, Naibu Waziri Khamis
alisema Serikali imeanza kuandaa miradi 11
ili kukabiliana na changamoto za kimazingira ambayo ni kusafisha mito na maziwa
kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Alisema changamoto ya magugu maji imeendelea kutatuliwa katika maeneo yaliyoathiriwa huku akiwataka wananchi kuendelelea kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha.
Akiendelea kujibu maswali Naibu Waziri Khamis alilieleza Bunge kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinazishirikiana katika kuhakikisha changamoto za kimazingira zinatatuliwa.
Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wafuate Sheria ya Mita 60 kwa kutofanya shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji zikiwemo kilimo kisicho endelevu, uvuvi usio endelevu
No comments:
Post a Comment