
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa Wahariri Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ukumbi wa Nane Nane, Mkoani Morogoro, ambapo aliwasihi kutumia jukwaa hilo kama fursa muhimu ya kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu, na pia kushauri juu ya masuala ya usimamizi wa shughuli za mnyororo wa ugavi.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, wakimskiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Mafunzo kwa Wahariri hao kuhusu masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma, katika ukumbi wa Nane Nane, Mkoani Morogoro, ambapo aliwasihi kutumia jukwaa hilo kama fursa muhimu ya kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu, na pia kushauri juu ya masuala ya usimamizi wa shughuli za mnyororo wa ugavi.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, wakimskiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Mafunzo kwa Wahariri hao kuhusu masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma, katika ukumbi wa Nane Nane, Mkoani Morogoro, ambapo aliwasihi kutumia jukwaa hilo kama fursa muhimu ya kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu, na pia kushauri juu ya masuala ya usimamizi wa shughuli za mnyororo wa ugavi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (Katikati alieketi), Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga (kushoto alieketi), Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, Bw. Ben Mwang'onda (kulia alieketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, baada ya hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma, iliyofanyika katika katika ukumbi wa Nane Nane, Mkoani Morogoro.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)
Na. Josephine Majura na Joseph Mahumi, WF, Morogoro
Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imefanya mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika sekta ya umma.
Akizungumza wakati akifungua rasmi mafunzo hayo, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizaravya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa programu shirikishi kati ya Wizara ya Fedha na wadau wake ikiwemo Sekta ya Habari, yenye lengo la kufikisha elimu sahihi kwa jamii kupitia wanahabari.
"Nafurahi kuona ushirikiano kati ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa vyombo vya habari ukiendelea kukua siku hadi siku pia Nimefarijika sana kuona mmeitikia vyema wito wa kushiriki katika mafunzo haya na mwitikio huu unaonesha dhamira ya pamoja ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano huu," alisema Bi. Omolo.
Alisisitiza kuwa, mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wanahabari kupata maarifa ya kina kuhusu shughuli zote muhimu zinazounda mnyororo wa ugavi kama vile ununuzi, usambazaji, uhifadhi, matumizi na uondoshaji wa bidhaa na huduma ndani ya taasisi za Serikali.
Bi. Omollo alifafanua kuwa, mafunzo hayo yanalenga kuwahusisha moja kwa moja wanahabari ili kusaidia kutoa taarifa sahihi, za wakati na zenye kuelimisha wananchi katika eneo la mnyororo wa ugavi kwa kuwa Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kikamilifu kupitia mnyororo wa ugavi.
“kwa mfano, zaidi ya asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali ya 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29, shilingi trilioni 35.2 zinatumika katika kununua vifaa na vitendeakazi mbalimbali, kulipia kandarasi za ujenzi na pia huduma ambazo zinawafikia wananchi walaji” alisisitiza Bi. Omolo.
Aliwasihi Wahariri na wanahabari kwa ujumla kulitumia jukwaa hilo kama fursa muhimu ya kujifunza, kujadili na kubadilishana uzoefu, na pia ushauri juu ya masuala ya usimamizi wa shughuli za mnyororo wa ugavi, ili kujiweka katika nafasi nzuri sana ya kuhabarisha umma kwa usahihi kupitia vyombo vyenu vya Habari.
Naye Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga, alisema kuwa kupitia kalamu za wanahabari, sauti, picha, na majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari, elimu kuhusu nafasi na mchango wa mnyororo wa ugavi katika maendeleo ya Taifa itafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alifafanua kuwa mnyororo wa ugavi unaanzia katika upangaji wa mahitaji, ununuzi, ugomboaji na uondoshaji, upokeaji, uhifadhi, usambazaji, hadi matumizi na uondoshaji wa bidhaa, vifaa au huduma.
Dkt. Mwakibinga alisema kuwa, kukosekana kwa usimamizi madhubuti katika hatua yoyote kati ya hizo kunaweza kusababisha hasara kubwa kwa Serikali, upotevu wa rasilimali, au huduma duni kwa wananchi.
“Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini tutaendelea kushirikiana nanyi kwa lengo mahsusi la kutoa uelewa mpana kuhusu shughuli za mnyororo wa ugavi kwa wadau muhimu wa mawasiliano kwa umma, ninyi Wahariri na waandishi wa habari.
Naye Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari katika mafunzo hayo, Bw. Ben Mwang'onda, aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatakua daraja la mahusiano kati ya Wizara hiyo na Umma katika kutoa taarifa kuhusu Mnyororo wa Ugavi.
"Kupitia mafunzo haya, tunaweza kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi, jambo ambalo linasaidia kuongeza uelewa wa umma na kuhamasisha uwajibikaji serikalini," alisema Bw. Mwang’onda.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, alisema kuwa Ushirikiano kati ya Wizara na Wanahabari umeendelea kuwa thabiti na imara na unaashiria matokeo mazuri ya elimu kwa umma.
“Tunaimani mafunzo haya ni mwendelezo wa Wizara wa kuangazia njia mbalimbali za kuelemisha umma kuhusu sera, program na matukio mbalimbali yanayofanywa na Wizara na niwasihi muendelee kushirikiana nasi ili kufikisha yale yanayofanywa na Serikali kwa wananchi” alisema Bw. Mwaipaja.
MWISHO
No comments:
Post a Comment