Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Muungano wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar Dk Said Gharib Bilal akifungua Mkutano wa ushawishi na utetezi na kubadilishana uzoefu huko Jumuiya hiyo Mpendae .
Baadhi ya washiriki wakimsikliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Muungano wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar Dk Said Gharib huko katika Jumuiya hiyo Mpendae .
Muungano wa Jumuiya ya maradhi yasioambukiza Zanzibar (Z-NCDA) imeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mkakati wake wa kupima afya kwa Jamii ili kupambana na maradhi yasioambukiza nchini.
Akitoa kauli hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya hiyo, Dk Said Gharib Bilal katika Mkutano wa ushawishi na utetezi na kubadilishana uzoefu juu ya kupambana na maradhi yasioambukiza katika Jumuiya ya Umoja wa watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza, Mpendae .
Amesema mkakati huo ni hatua muhimu na ya kupongezwa, kwani utasaidia kugundua mapema magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, saratani na maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakiongezeka siku Hadi siku na kusababisha vifo.
Amesema juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya, itasaidia wananchi kupatiwa tiba kwa haraka na kuokoa Maisha yao.
Aidha amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kupambana na maradhi hayo jambo ambalo litasaidia kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
Dkt Said ameahidi kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya ili kuhakikisha watu Wanapatiwa elimu sahihi juu ya Maradhi hayo pamoja na njia ya kukabiliana nayo.
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Louis H. Majaliwa alisema maradhi yasioambukiza yamekuwa kwa kasi hapa Zanzibar kutokana na wananchi kutokukubali kubadili mfumo wao wa maisha.
Hivyo aliitaka Jamii kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kugundulika tatizo mapema na kupatiwa matibabu Kwa haraka .
Naye Meneja wa Jumuiya hiyo Haji Khamis Fundi amesema kupitia mradi wa mkakati imeweza kuwapatia elimu ya maradhi yasioambukiza Wadau Mbali mbali Kwa lengo la kufikisha kwa Jamii wakiwemo Waandishi wa Habari wasanii watunga sera pamoja na watetezi dhidi ya maradhi ya kisukari.
na maradhi yasioambukiza
Kwa Upande wa watu wanaoishi na maradhi hayo ameishukuru Serikali Kwa kujenga vituo vya afya mbali mbali jambo ambalo limerahisishia upatikanaji wa huduma za matibabu hayo .
Mkutano huo umehusisha Wadau mbali mbali ikiwemo Madaktari , Waandishi wa Habari, watu wanaoishi na maradhi pamoja na Jumuiya wanachama.
No comments:
Post a Comment